AMUUA MKEWE NA KULALA NA MAITI KWA SIKU 3


Polisi katika Wilaya ya Kyegegwa nchini Uganda, wamemkamata mwanaume mwenye umri wa miaka 47, kwa tuhuma za kumuua mke wake aliyetambuliwa kwa jina Twikirize Ronious.

Kulingana na msemaji wa polisi wa Rwenzori Magharibi Vincent Twesige, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 23, aliuawa usiku wa Novemba 11, wakati wa ugomvi wa nyumbani.

Daily Monitor inaripoti kuwa usiku huo wa tukio hilo, majirani walimsikia mshukiwa akimpiga mke wake ambaye alikuwa akiishi naye katika nyumba ya kupanga.

Ikizingatiwa kwamba wawili hao wana mazoea ya kupigana, majirani walipuuza na hawakuingilia kati lakini walibaini mnamo Novemba 12, kuwa nyumba ya wanandoa hao ilikuwa imefungwa.

Waliongeza kuwa hawakushuku chochote kibaya kwani walifikiri wawili hao walikuwa wamesameheana kama kawaida na walikuwa wameenda kulima pamoja.

Hata hivyo, mashaka yao yaliongezeka walipogundua kwamba nyumba hiyo ilifungwa kwa muda mrefu hali ambayo haikuwa ya kawaida.

Majirani hao walifichua kuwa walipompigia simu mshukiwa, aliwadanganya kuwa alikuwa na Twikirize bustanini.

Licha ya uwongo wake, waliomba msaada kutoka kwa viongozi wa eneo hilo ambao pamoja na dada yake wa marehemu walimpigia simu mkwe wake ambaye alikataa kujibu.

"Mnamo Novemba 15, mshukiwa alikiri kumuua mkewe na kuongeza alikuwa ndani ya nyumba na mwili wa mkewe," polisi walieleza.

Jambo la ajabu katika tukio hilo ni kwamba polisi walipovamia nyumba hiyo, walimpata mshukiwa amekula sumu na alikuwa amelala kitanda kimoja na maiti ya mke wake.

Twesige aliongeza kuwa mshukiwa alipelekwa hospitalini kwa matibabu huku mwili wa mke wake ukihamishiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Kyegegwa kwa uchunguzi wa maiti.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post