WATANZANIA KUSHINDA ZAWADI NONO KOMBE LA DUNIA


Macho ya ulimwengu mzima yamegeukia huko nchini Qatar kushuhudia mataifa 32 yakichuana kuwania Kombe la Dunia. Raia kutoka nchi washiriki na wapenzi wa michezo kote ulimwenguni wanazidi kufuatilia kwa karibu zaidi kadri michuano hiyo inavyozidi kwenda katika hatua za juu.


Tanzania kama ilivyo kwa mataifa mengine ambayo hayakufuzu kwa michuano hiyo haina ushiriki wa moja kwa moja. Hata hivyo mashabiki wa michezo nchini Tanzania wanafuatilia michuano hiyo kwa ukaribu sana na kushiriki kwa njia mbalimbali. Wengi wao wamechagua kuwa mashabiki wa timu za nchi wanazozipenda huku wengine wakishiriki katika mashindano mbalimbali ya bahati nasibu na ubashiri kama sehemu ya kufurahia zaidi michuano hiyo inayofuatiliwa zaidi duniani.


Ili kuhamasisha Watanzania wengi zaidi, Betway Tanzania imeungana na Airtel Tanzania kutambulisha shindano la ubashiri ambazo zitawawezesha wapenzi wa soka wanaofuatilia kombe la dunia kujishindia zawadi mbalimbali. Shindano hilo ambalo limepangwa kufanyika kwa kipindi chote cha kombe la dunia itawanufaisha washiriki kwa mfumo ulioelezewa hapa chini;


Zawadi ya kila siku ya fedha taslimu shilingi 10,000 kwa washindi 50; Watu 50 watakuwa na nafasi ya kushinda shilingi 10,000 kila siku.

Zawadi ya kila wiki ya fedha taslimu shilingi 1,000,000; kila wiki mtu mmoja atakuwa na nafasi ya kuibuka na kitita cha shilingi 1,000,000. Hii ina maana kwa kipindi kilichosalia cha mashindano angalau watu wanne wana nafasi ya kushinda zawadi ya pesa taslimu ya shilingi 1,000,000.

Zawadi kubwa ya shilingi 5,000,000; mshindi wa jumla anatarajiwa kukusanya jumla ya shilingi 5,000,000 zitakazotolewa baada ya fainali ya kombe la dunia.


Sambamba na zawadi za pesa taslimu, mashabiki wa michezo pia wana nafasi ya kupata dau la bure la kuwasaidia kubashiri bila malipo. Hii itaongeza nafasi za mashabiki wengi zaidi kushiriki katika shindano hili na kuibuka mshindi wa kila siku, mshindi wa wiki au mshindi wa jumla.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shindano hilo, Meneja Uendeshaji wa Betway Tanzania, Jimmy Masaoe alisema kupitia shindano hilo wateja wa Betway wataendelea kuvuna matunda ya kombe la dunia kwa kuwa tayari wamekuwa wakifurahia mashindano hayo kupitia huduma nyingine za Betway.


"Kwa wateja wetu wapendwa wa Betway, hii ni nyongeza. Ni faida ya ziada kwa wateja wanaotumia Airtel Money kwa sababu wanaweza kujishindia zawadi kadha wa kadha kadiri wanavyobashiri nasi kupitia Airtel Money. Shindano hii ni maalum kwa ajili ya kombe la dunia na tutakuwa na washindi 50 kila siku, mshindi mmoja kila wiki na mshindi wa jumla wa zawadi kuu ya shilingi 5,000,000,” alisema Masaoe.


Masaoe alisisitiza kuwa huduma ningine za ubashiri chini ya Betway zinandeleea na ametoa wito kwa mashabiki wa michezo kuendelea kufurahia huduma bora zinazotolewa na Betway.


Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda amesema watumiaji wa huduma za Airtel Money wanaweza kupata kilicho bora zaidi katika kombe la dunia kwa kutabiri matokeo katika hatua zote za mashindano hayo.


“Tumefurahi sana kushirikiana na Betway Tanzania kwa sababu tunajua kupitia ushirikiano huu watumiaji wetu wa huduma ya Airtel Money wanaopenda michezo watanufaika moja kwa moja na kombe la dunia. Lengo letu kama ilivyokuwa siku zote ni kuhakikisha wateja wetu wanapata kilicho bora zaidi kutoka kwenye huduma zetu. Katika kipindi hiki muhimu ambacho macho ya ulimwengu mzima yako kwenye michuono hiyo, tunatamani kuona wateja wetu wakinufaika na kombe la dunia na tunaamini hii ni njia mojawapo ya kuwasaidia,” alisema Nchunda.


Aliongeza kuwa shindano hilo pia ni sehemu ya ofa za msimu wa sikukuu kutoka kwa kampuni hiyo ya mawasiliano ya simu kwani Airtel imedhamiria kusherehekea msimu wa sikukuu na wateja wake wapendwa.


Huku timu tatu pekee zikiwa zimefuzu kwa hatua ya 16 bora hadi kufikia Jumatatu, Novemba 28, 2022, mashabiki wa michezo bado wanaweza kufanya ubashiri wao katika michezo inayoendelea ya hatua ya makundi ili kujiwekea nafasi ya kushinda zawadi. Zawadi kuu ya shilingi 5,000,000 itatolewa kwa mshindi tarehe 31 Disemba baada ya mchezo wa fainali utakaochezwa Disemba 18, 2022.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post