WAIGIZAJI MAARUFU WAKAMATWA WAKIANDAMANA IRAN


Muigizaji maarufu nchini Iran Hengameh Ghaziani

WAIGIZAJI wawili wa kike mashuhuri nchini Iran wametiwa hatiani na mamlaka nchini humo kwa kosa la kuandamana kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu.

Hengameh Ghaziani na Katayoun Riahi wameonekana hadharani pasipokuwa na Hijab ikiwa ni sehemu ya kuonesha kuunga mkono kwao kwa waandamanaji na wanaharakati wanaopinga sheria kandamizi nchini humo.



Kwa mujibu wa shirika la Habari la Irna limebainisha kuwa waigizaji hao wamefanya hivyo ikiwa ni muendelezo wa kupinga muendelezo wa sheria kandamizi za kimaadili nchini humo huku tukio kubwa la kuuawa kwa Mahsa Amini (22) kwa kosa la kutovaa Hijab likitajwa kuwa sehemu ya mambo yaliyowakasirisha wananchi wa Iran ambao wameamua kuandamana kupinga unyanyasaji huo.



Mahsa Amini alikamatwa na Polisi wa Tehran Septemba 16, 2022 kwa kosa la kutovaa Hijab na akawekwa mahabusu lakini siku tatu baadaye akaripotiwa kufariki.Hengameh Ghaziani alionekana hadharani akiwa hajavaa Hijab ikiwa ni ishara ya kuunga mkono sheria kandamizi nchini humo zinazohusiana na maadili

Kulikuwa na ripoti kuwa Mahsa alipigwa na kitu Kizito kichwani na Afisa wa Polisi lakini Polisi walikanusha taarifa hizo na kudai kuwa Mahsa alipata shambulio la Moyo (Heart attack).


Kabla ya kukamatwa Hengameh Ghaziani aliandika katika ukurasa wa mtandao wake wa kijamii kuwa:

“Kwa chochote kile kinachoweza kutokea, tambueni kuwa kama ilivyo siku zote ntaendelea kuwa pamoja na watu wa Iran.”



Alimaliza kwa kuongeza kuwa, “ Hili linaweza kuwa ndiyo chapisho langu la mwisho.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post