TGNP YATOA ELIMU YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WANAFUNZI WA KIUME SHULE YA MSINGI NA SEKONDARI LUNGUYA

 Afisa Programu kutoka TGNP, Jackson Malangalila akitoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Lunguya na Sekondari Lunguya halmashauri ya Msalala.

Na Kadama Malunde - Malunde  1 blog

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umetoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa vijana wa kiume wanaosoma katika shule ya Msingi na Sekondari Lunguya zilizopo katika kata ya Lunguya Halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga pamoja na kuwawezesha kutengeneza mipango kazi ya kupinga ukatili wa kijinsia shuleni na katika jamii zao.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo Alhamisi Novemba 17,2022 katika Shule ya Msingi Lunguya, Afisa Programu kutoka TGNP, Jackson Malangalila amesema lengo ni kuwahusisha wavulana katika kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia na kuwawezesha wavulana hao kuwa sehemu ya kuondoa ukatili wa kijinsia kwa wasichana.

"Mafunzo haya ambayo yamehudhuriwa na wanafunzi 74 wa kiume pia yanalenga kuwafundisha njia mbalimbali za kuondoa ukatili ikiwemo kuwaunganisha na  Watoa huduma za kisheria, vituo vya taarifa na maarifa, viongozi wa serikali na wadau mbalimbali", amesema Malangalila.

Naye Mraghbishi kutoka TGNP Hancy Obote amesema Ukatili wa kijinsia haukubaliki katika jamii hivyo ni lazima kila mmoja apige vita vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia.

"Toeni taarifa kwa viongozi wa serikali za mitaa na vituo vya taarifa na maarifa na viongozi mbalimbali ili kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia",amesema Obote.
Afisa Programu kutoka TGNP, Jackson Malangalila akitoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Lunguya na Sekondari Lunguya halmashauri ya Msalala leo Alhamis Novemba 17,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Programu kutoka TGNP, Jackson Malangalila akitoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Lunguya na Sekondari Lunguya halmashauri ya Msalala 

Mraghbishi kutoka TGNP Hancy Obote akitoa elimu ya Ukatili wa Kijinsia kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Lunguya na shule ya Sekondari Lunguya zilizopo katika Halmashauri ya Msalala Mkoa wa Shinyanga.

Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma ya Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija akitoa elimu kuhusu sheria za Watoto na Elimu pamoja na ukatili wa Kijinsia

Mwanafunzi wa shule ya msingi Lunguya Baraka Nicholaus akielezea namna watavyoshiriki katika kutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwemo kutatoa taarifa za ukatili kwa viongozi
Mwanafunzi shule ya Sekondari Lunguya Juma Yohana akielezea namna watakavyoshiriki kutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwemo kuunda Gender Club shuleni.
Wanafunzi wakifuatilia elimu ya ukatili wa kijinsia 

Mwanafunzi akichangia hoja wakati elimu ya ukatili wa kijinsia ikitolewa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post