GGML YANG’ARA TUZO ZA TRA

KAMPUNI ya Geita Gold Mining Ltd. (GGML) imetambuliwa kwa mara nyingine tena kama mlipa kodi wa viwango vya juu katika sekta ya madini kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Tuzo hizo zilipokelewa mwishoni mwa wiki na Meneja Mwandamizi wa Fedha kutoka GGML, Ikingo Gombo  na Meneja Utatuzi wa Migogoro ya Kodi kutoka GGML, Godvictor Lyimo kutoka kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano, Nape Nnauye.


Pia imetambuliwa kama kampuni iliyozingatia kiwango bora cha thamani ya bidhaa zilizosafirishwa nje ya nchi mwaka 2021/2022. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Chande  alikabidhi tuzo hiyo kwa Meneja Mwandamizi wa Fedha kutoka GGML, Ikingo Gombo na Meneja Utatuzi wa Migogoro ya Kodi Godvictor Lyimo kutoka GGML.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post