BOMU LAUA NA KUJERUHI KIGOMA


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma ACP Filemon Makungu

***
Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Amosi Petro mwenye umri wa miaka 45 mkulima na mkazi wa kijiji na kata ya Basanza Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma, ameuawa kwa kulipukiwa na bomu la kutupwa kwa mkono huku wengine wawili wakijeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Uvinza.


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma ACP Filemon Makungu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba bomu hilo lilitupwa katika chumba cha kuuza pombe za kienyeji ambapo marehemu na majeruhi walikuwa wameketi wakiendelea kunywa pombe kisha kulipukiwa.


ACP Makungu amebainisha kuwa chanzo cha tukio hilo kinahusisha migogoro ya kifamilia na kwamba tayari mtu mmoja amekamatwa kwa tuhuma za kuhusika na tukio.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi Mkoani Kigoma wameeleza juu ya tukio hilo na kuomba uchunguzi ufanyike wa haraka kujua chanzo cha tukio.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post