LORI LAGONGA MAGARI MAWILI NA KUUA, KUJERUHI DAR


Magari yaliyopata ajali

Mtu mmoja amepoteza maisha na wengine wawili kujeruhiwa kwenye ajali iliyosababishwa na lori lililobeba saruji kufeli break na kuyagonga magari mawili madogo barabara ya Wazo Tegeta Dar es Salaam.

Shahidi aliyeshuhudia ajali hiyo, anaeleza kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 1 asubuhi katika barabara ya Wazo Tegeta jijini Dar es Salaam, na hapa anasimulia zaidi.

Aidha wananchi wameiomba serikali kufanya upanuzi wa barabara hiyo, ili kupunguza ajali na msongamano wa magari katika barabara hiyo, yenye watumiaji wengi.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Mtatiro Kitinkwi, amesema katika ajali hiyo kifo ni kimoja na majeruhi wawili ambao walipelekwa hospitali ya Kitengule, na baadaye kupelekwa Muhimbili.

Aidha ACP Mtatiro ameeleza kuwa dereva wa lori hilo, Bw.Said Salim Omari mwenye umri wa miaka 29, mkazi wa Wazo anashikiliwa na Jeshi hilo kwa hatua zaidi za kisheria.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post