WAZIRI MKENDA AONGOZA HARAMBEE UNUNUZI KIWANJA CHA KANISA ROMBO//AWEZESHA KUPATIKANA MIL 82.8

 
Waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda.

*Na Mathias Canal, Rombo-Kilimanjaro*


Mbunge wa Jimbo la Rombo Mkoani Kilimanjaro ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda leo tarehe 2 Octoba 2022 ameongoza harambee ya ununuzi wa kiwanja cha Parokia ya Mtakatifu Pius X Tarakea Jimbo katoliki Moshi.


Katika harambee hiyo kiasi cha Shilingi 82,841,900 kimepatikana ambapo ahadi ni Shilingi 36,313,000 na fedha taslimu zilizopatikaa ni Shilingi 46,528,900.


Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa harambee hiyo Waziri Mkenda amewapongeza waumini wote kwa kazi kubwa na nzuri ya kuendelea kujitolea kwa ajili ya maendeleo endelevu ya kanisa.


Prof Mkenda amewahakikishia wananchi wa Rombo na waumini wa Parokia ya Mtakatifu Pius X Tarakea Jimbo katoliki Moshi kuwa ofisi ya mbunge itaendeleza ushirikiano kwa ajili ya shughuli zote za maendeleo ya kanisa.


Kadhalika, Waziri Mkenda ametoa rai kwa Kanisa kuendelea kushirikiana na serikali kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wote.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post