ST.MARY’S MBEZI BEACH YAPONGEZWA KWA MAENDELEO YA TAALUMA

Wanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya St Mary’s Mbezi Beach jijini Dar es Salaam wafurahia na wenzao kwenye mahafali yao yaliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki. Wanafunzi wa shule ya sekondari ya St Mary’s Mbezi Beach wakionyesha mitindo ya mavazi kwenye mahafali ya kidato cha nne ya shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo. Meneja Miradi wa Kilua Group, Amannzy Mohamed akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya St Mary’s Mbezi Juu jijini Dar es Salaam hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo. Wengine ni viongozi wa shule hiyo. Mwenyekiti wa Bodi ya shule za St Mary’s Dallas Mhoja akizungumza kwenye mahafali ya kidato cha nne ya shule hiyo yaliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki.

Sehemu ya walimu wa shule za St Mary’s wakitambulishwa kwenye mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo mwishoni mwa wiki

************************

Na Mwandishi Wetu

WAZAZI wameshauriwa kufuatilia kwa karibu maendeleo ya watoto wao kitaaluma na tabia ili waweze kufanya vizuri kwenye mitihani huku shule ya St Mary’s Mbezi Beach ikipongezwa kwa mafanikio ya kitaaluma.

Pongezi hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki na Meneja Miradi wa Kilua Group, Ammanzy Mohamed kwenye mahafali ya kidato cha nne ya shule ya sekondari ya St. Mary’s Mbezi Beach, yaliyofanyika shuleni hapo Mbezi Beach.

Alisema wazazi hawapaswi kuwaachia kazi ya kufuatilia mienendo ya tabia na taaluma walimu bali nao wanawajibika kufuatilia kila mara kuangalia kama wanafanya vizuri kitaaluma na wanapogundua mwenendo mbaya watoe taarifa.

Alisema wazazi wanapaswa kutengeneza urafiki wa karibu na walimu wa watoto wao ili wawe wanapata mrejesho wa kinachoendelea badala ya kuwaacha tu baada ya kulipa ada.

“Nimefurahi kuona vipaji vya aina mbalimbali hapa St Mary’s na na nawapongeza walimu kwa kazi nzuri sana ya kuwalea na kuwafundisha vijana wetu kiasi cha kufanya vizuri kiasi hiki lakini ninachosisitiza sisi wazazi tushirikiane na walimu kufuatilia tabia za watoto wetu,” alisema

“Kwa maonyesho tuliyoona hapa inaonekana hawa wanafunzi watafanya vizuri sana kwenye mtihani wao wa mwisho na nimesikia hapa wanavyozungumza kingereza kilichonyooka na kifaransa kizuri sasa hivi vipaji lazima vifuatiliwe na vilelewe,” alisema Ammanzy.

Naye Mkuu wa Sekondary ya Mbezi, Ntipoo Reca alisema tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2001 chini ya mwanzilishi wake Dk. Getrude Rwakatare, shule zimekuwa zikijitahidi kuzalisha wahitimu wenye maadili na walioiva kitaaluma.

Alisema shule hiyo imejitahidi kuweka madarasa ya kutosha ili kila darasa liwe na wanafunzi 25 pekee ili kuhakikisha mwalimu anakuwa na uwezo wa kumfikia kila mwanafunzi wake.

Alisema pamoja na kuweka madarasa ya kutosha uongozi wa shule umejitahidi kuweka walimu mahiri na wabobezi wa kutosha kwa masomo wanayofundisha hali ambayo imewawezesha wanafunzi kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya kitaifa.

Alisema uongozi wa shule umejitahidi kuweka maktaba kubwa iliyosheheni vitabu kwa wanafunzi wa michepuo yote na maabara kubwa inayowawezesha wanafunzi wa masomo ya sayansi kusoma kwa vitendo masomo yao.

“Na kwa nidhamu hapa St Mary’s tumeweza kwa asilimia kubwa kuwajenga kuwa na nidhamu ya masomo na muda kwasababu wanafuata ratiba zao za masomo za kila siku bila kushurutishwa na mtu na kwenye mtihani wa mwaka huu tuna uhakika wa kutoa daraja la kwanza na la pili tu,” alisema Reco.

Naye Ofisa Elimu Kata ya Mbezi Juu, Clarence Makule alipongeza shule hiyo kwa maendeleo yake ya kitaaluma na aliwataka wasibweteke na mafanikio wanayoyapata bali waendelee kuhakikisha wanafunzi wao wanafaulukwa alama za juu na kushika nafasi za juu kitaifa.

“Walimu wao ni wazuri sana na wengine wamesomea hapahapa kuanzia shule ya awali na wamefanikiwa kuja kufundisha hapa mimi kama ofisa elimu nawapongeza kwa kazi nzuri ila wasibweteke kwa sababu ushindani ni mkubwa walimu wasome kwa bidii na walimu watimize wajibu wao,” alisema

Alisema wanafunzi wa shule hiyo wanapewa nafasikuonyesha vipaji vyao kwenye mambo mbalimbali ikiwemo michezo na aliwapongeza kwa namna wanavyoshirikiana na serikali katika maendeleo ya taaluma yao.

“Shule ni nzuri tunawaalika wazazi walete watoto wao, shule hii ilikuwa na wanafunzi wachache ila kutokana na kufanya vizuri kitaaluma sasa idadi ya wanafunzi inaongezeka na mimi kama ofisa elimu Kata ya Mbezi Juu nawahakikishia wazazi shule iko vizuri wawalete St Mary’s,” alisema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post