POSTA DODOMA YAADHIMISHA SIKU YA POSTA DUNIANI KWA KUTOA MSAADA HOSPITALI YA RUFAA YA DODOMA


MENEJA Msaidizi wa Shirika la Posta mkoa wa Dodoma Bw.Steven Kibono (kushoto) akimkabidhi Afisa Muuguzi Msaidizi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Mulagwa Mulagwa msaada wa vyandarua 100 walivyokabidhi katika hospitali hiyo zenye thamani ya shilingi milioni moja katika kuadhimisha siku ya Posta Duniani iliyofanyika leo Oktoba 9,2022.


MENEJA Msaidizi wa Shirika la Posta mkoa wa Dodoma Bw.Steven Kibono akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika hilo mara baada ya kukabidhi msaada wa vyandarua 100 zenye thamani ya shilingi milioni moja katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma katika kuadhimisha siku ya Posta Duniani iliyofanyika leo Oktoba 9,2022.


WAFANYAKAZI wa Shirika la Posta mkoa wa Dodoma wakitoa pole kwenye wodi ya watoto baada ya kukabidhi msaada wa vyandarua 100 zenye thamani ya shilingi milioni moja katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma katika kuadhimisha siku ya Posta Duniani iliyofanyika leo Oktoba 9,2022.


MENEJA Msaidizi wa Shirika la Posta mkoa wa Dodoma Bw.Steven Kibono,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada wa vyandarua 100 zenye thamani ya shilingi milioni moja katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma katika kuadhimisha siku ya Posta Duniani iliyofanyika leo Oktoba 9,2022.


Msimamizi wa shughuli za masoko Mkoa wa Dodoma Posta Bw.Philipo Kowero,akielezea mikakati ya shirika hilo mara baada ya kukabidhi msaada wa vyandarua 100 zenye thamani ya shilingi milioni moja katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma katika kuadhimisha siku ya Posta Duniani iliyofanyika leo Oktoba 9,2022.


Afisa Muuguzi Msaidizi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Mulagwa Mulagwa,akitoa pongezi kwa Shirika la Posta Mkoa wa Dodoma mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vyandarua 100 zenye thamani ya shilingi milioni moja ikiwa ni kuadhimisha siku ya Posta Duniani iliyofanyika leo Oktoba 9,2022.


Mfanyakazi wa Shirika la Posta Mkoa wa Dodoma Bi.Pendo Japhet,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya shirika hilo kutoa msaada wa vyandarua 100 zenye thamani ya shilingi milioni moja katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma katika kuadhimisha siku ya Posta Duniani iliyofanyika leo Oktoba 9,2022.


VIONGOZI pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Posta mkoa wa Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuadhimisha siku ya posta Duniani kwa kutoa msaada wa vyandarua 100 zenye thamani ya shilingi milioni moja katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

.................................................

Na Alex Sonna-DODOMA

KATIKA kuadhimisha siku ya Posta Duniani,Shirika la Posta Mkoani Dodoma limetoa msaada wa vyandarua 100 hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma zenye thamani ya shilingi milioni moja lengo likiwa ni kurudisha kwa jamii kile ambacho wanakipata.

Akizungumza leo Oktoba 9,2022 jijini Dodoma wakati wa utoaji wa vyandarua hivyo,katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma,Meneja Msaidizi wa Shirika hilo ,Steven Kibono amesema wameamua kufanya hivyo ili kurudisha kwa jamii kile ambacho wanakipata.

Amesema hospitali hiyo ni wadau wao kutokana na kusafirisha sampuli mbalimbali kupitia shirika hili.

“Huduma zetu siku hizi zimeboreshwa zimebadilika kutoka manual sasa hivi tunafanya mambo kidigital tuna mfumo mpya ambao tunautumia ambao unatuwezesha mteja yoyote hata akiwa nyumbani kwake anapata huduma pamoja na kununua vitu online,”amesema Kibono.

Naye,Msimamizi wa shughuli za masoko Mkoa wa Dodoma Posta Bw.Philipo Kowero, amesema wanaadhimisha siku ya Posta Duniani na kwa mwaka huu wamekabidhi msaada katika wodi ya watoto.

“Kwa kweli kwetu ni fahari na faraja kubwa kurudisha kwa jamii kile ambacho wamekuwa wakichangia katika shirika hili la uuma.Tunaunga mkono jitihada za Serikali katika kutokemeza ugonjwa wa Malaria hivyo tukaona tutoe msaada huu,”amesema Kowero,

Amesema wanaushukuru uongozi wa shirika kwa jitihada wanazoendelea nazo za katika mageuzi ndani ya shirika kwani kuna mabadiliko mengi yamejitokeza.

Kwa upande wake Afisa Muuguzi Msaidizi wa hospitali hiyo Mulagwa Mulagwa amesema wanashukuru Shirika la Posta kwa msaada ambao wameupeleka katika hospitali hiyo.

“Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Hospitali tunashukuru sana Shirika la Posta kwa hichi ambacho wamekiona ni cha muhimu Mungu awabariki sana maana vyandarua hivi vitawasaidia wagonjwa ambao wapo mawodini ambao wamelazwa,”amesema Mulagwa

Hata hivyo, ametoa wito kwa taasisi zingine kujitokeza kujitolea kama shirika hilo lilivyofanya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post