NEWALA MJI YAANZA KUTEKELEZA MAAGIZO YA WAZIRI WA ARDHI

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Newala mkoani Mtwara Shamim Daudi Mwariko (kulia) alikabidhiwa hatimiliki za ardhi saba na Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mtwara Rehema Mwinuka mkoani Mtwara jana.
Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mtwara Rehema Mwinuka (kulia) akimsikiliza mmoja wa wateja wakati Ofisi ya Ardhi Mkoa ilipotoa huduma jumuishi za sekta ya ardhi. Watumishi wa sekta ya ardhi wakitoa huduma za ardhi katika kituo jumuishi Mtwara.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mtwara Rehema Mwinuka akiwa katika picha ya pamoja na wananchi aliowakabidhi hati (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

**************************

WANMM, MTWARA

Halmashauri ya Mji wa Newala mkoa wa Mtwara imeanza kutekeleza maagizo ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula ya kuzitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha zinapima na kumilikishwa maeneo yake yakiwemo ya shule, zahanani na vituo vya mabasi ili kuepuka migogoro ya ardhi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Newala Shamim Daudi Mwariko alikabidhiwa jumla ya hati saba na Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mtwara Rehema Mwinuka ambapo hati tano kati ya alizokabidhiwà ni za shule za msingi na hati mbili ni za zahanati.

Shule za msingi zilizopata hatimiliki za ardhi ni Mtangalanga, Kiduni, Butiama, Mcholi II na Mkoma I huku upande wa zahanati zikiwa ni Mkoma I na ile ya Makondeko.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi hati hizo mkoani Mtwara jana Kamishna wa Ardhi mkoa wa Mtwara Rehema Mwinuka aliipongeza halmashauri ya Mji wa Newala kwa uamuzi wa kupimiwa maeneo yake na kuzitaka halmashauri nyingine katika mkoa huo kuiga mfano wa halmashauri hiyo kwa kupima na kumilikishwa maeneo yake ili kuepuka uvamizi katika maeneo hayo.

"Nichukue fursa hii kuwapongeza halmashauri ya Mji wa Newala kwa uamuzi wenu wa kupima maeneo yenu, hii itasaidia sana kupunguza migogoro ya ardhi inayotokana na uvamizi na niombe hakmashauri nyingine ziige mfano wenu" alisema Rehema.

Mbali na kukabidhi hati kwa halmahauri ya Mji wa Newala kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mtwara aliwaongoza watumishi wa mkoa wake kutoa hati kwa wamiliki wa ardhi waliokamikisha taratibu za kupatiwa hati sambamba na kusikiliza na kutatua changamoto za sekta ya ardhi katila kituo jumuishi.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanzisha utaratibu wa ofisi zake za ardhi katika mikoa kuwa na vituo jumuishi vya kusikiliza na kutatua changamoto za ardhi pamoja na kutoa hatimiliki za ardhi ikiwa ni juhudi za kusogeza huduma karibu na wananchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments