WANAHARAKATI WATAKA SHERIA ZITUMIKE KUKOMESHA UKATILI WA KIJINSIA "MENGINE SIYO MILA NI ULAFI TU"

Afisa Mradi wa Elimu ya Haki za Binadamu kutoka Shirika la Tusonge CDO, Consolata Kinabo.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jamii imetakiwa kuacha tabia za kumaliza kesi za masuala ya ukatili wa kijinsia kienyeji ikiwemo mimba na ndoa za utotoni kwa kisingizio kuwa ni mila na desturi bali sheria inatakiwa kuchukua mkondo wake ili kukomesha matukio ya ukatili.

Rai hiyo imetolewa leo Alhamisi Oktoba 6,2022 na Afisa Mradi wa Elimu ya Haki za Binadamu kutoka Shirika la Tusonge CDO, Consolata Kinabo kwenye Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini wakati wa warsha iliyoongozwa na mada “Mila Kandamizi ni kikwazo cha kufikia haki za uchumi na maisha endelevu” katika viwanja vya Kwasa Kwasa wilayani Same.

“Tunakwepa kufuata sheria na tunamaliza kesi za ukatili wa kijinsia kienyeji. Tuna visingizio vya kusema mila na desturi zetu zinasema hivi matokeo yake wahanga wanazidi kuathirika na yanakuwa ni mazoea katika jamii kwa sababu wanaona hakuna sheria yoyote inayochukuliwa kwa wanaofanya ukatili”,amesema Kinabo.

Naye mmoja wa washiriki wa warsha hiyo,Sauda Hussein Mshana kutoka kituo cha taarifa na maarifa cha Kivule wilayani Same, amesema siyo kila tukio la ukatili wa kijinsia linatokana na mila na desturi kandamizi bali ni tabia tu ya mtu.

“Mambo mengine siyo mila bali ni ulafi tu, unampaje mimba mtoto? Unaoaje mtoto?, sheria zichukue mkondo wake ili haya mambo yakome”,amesema.

Washiriki wa warsha wamekemea vitendo vya ukeketaji kwa wanawake wakisema vinaleta madhara kwa wanawake ikiwemo kukosa ujasiri katika maisha, kupata maambukizi ya VVU, Homa ya Ini kwani vifaa vinavyotumika kufanyia ukeketaji siyo salama.
Afisa Mradi wa Elimu ya Haki za Binadamu kutoka Shirika la Tusonge CDO, Consolata Kinabo akizungumza kwenye Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini katika viwanja vya Kwasa Kwasa wilayani Same.
Afisa Mradi wa Elimu ya Haki za Binadamu kutoka Shirika la Tusonge CDO, Consolata Kinabo akizungumza kwenye Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini wakati wa warsha iliyoongozwa na mada “Mila Kandamizi ni kikwazo cha kufikia haki za uchumi na maisha endelevu” katika viwanja vya Kwasa Kwasa wilayani Same.

Mwakilishi kutoka  Shirika la NAFGEM Tanzania, Magdalena Mwile akizungumza kwenye Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini wakati wa warsha iliyoongozwa na mada “Mila Kandamizi ni kikwazo cha kufikia haki za uchumi na maisha endelevu” katika viwanja vya Kwasa Kwasa wilayani Same.

Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali akichangia hoja kwenye Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini wakati wa warsha iliyoongozwa na mada “Mila Kandamizi ni kikwazo cha kufikia haki za uchumi na maisha endelevu” katika viwanja vya Kwasa Kwasa wilayani Same.
Wadau wakiwa kwenye Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini wakati wa warsha iliyoongozwa na mada “Mila Kandamizi ni kikwazo cha kufikia haki za uchumi na maisha endelevu” katika viwanja vya Kwasa Kwasa wilayani Same.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments