MGANGA WA JADI AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA KWA MAUAJI YA WATOTO WAWILINa Walter Mguluchuma - Katavi

MAHAKAMA kuu kanda ya Sumbawanga imemuhukumu kunyongwa hadi kufa mganga wa jadi aitwaye James Kapyela (57) baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kufanya mauaji ya watoto wawili waliofahamika kwa majina ya Nicholaus Mwambage (7) pamoja na Emmanuel Juma (4).


Hukumu hiyo imetolewa jana na Jaji wa mahakama hiyo, Thadeo Menempazi ambaye amesema kuwa mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi 11 na hivyo ikaamua kutoa hukumu hiyo.


Upande wa Jamhuri ukiongozwa na mawakili Marieta Maguta akisaidiana na Wakili Saimon Peres ambao walidai mahakamani hapo kuwa tukio hilo lilitokea siku ya Machi 23/2019 Katika mtaa wa Vuta kitongoji cha Kizwite mjini Sumbawanga.


Wakili Peres ameiambia mahakama hiyo kuwa kabla ya kuthibitika kuwa watoto hao ameuawa, walipotea ambapo wazazi na majirani wa watoto hao walianza juhudi za kuwatafuta na Kisha kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi kilichopo mjini Sumbawanga.
Ilidaiwa mahakamani hapo siku iliyofuata Kuna binti alikua anakwenda mtoni kuchota maji na alimuona mtoto mmoja kati ya wale watatu waliopotea na akatoa taarifa kwa wazazi wake ambao baada ya kumuona aliwaeleza wazazi wake kule alikokuwa na kuaacha wenzake ambapo waliambatana naye kwa lengo la kwenda kuwatafuta.


Walipofika kwenye nyumba ya mtuhumiwa, wazazi hao walikuta kuna gari bovu ambalo lilikuwa limeegeshwa nje na walipo fungua mlango wa gari hilo walikuta ndani kukiwa kuna kinyesi cha binaadamu pamoja na harufu kali na nzi wengi.


Ilidaiwa kwamba ndipo wazazi hao walipo piga hatua kwenye moja ya Pagale lilipo karibu na nyumba ya Kapyela na ndani yake waliikuta miili ya watoto hao ikiwa imetupwa ndani ya jumba hilo. 

Inadaiwa baada ya uchunguzi wa kitabibu ilibainika kabla ya kunyongwa watoto hao walilawitiwa.

Hata hivyo baada ya mtuhumiwa kukutwa na hatia Wakili wa upande wa Mashitaka waliiomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye kufanya vitendo kama hivyo.


Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili,Deogratias Sanga huku mtuhumiwa akiwa hana mashaidi isipokuwa alikuwa peke yake ambapo alipewa nafasi ya kujitetea kabla ya mahakama kutoa hukumu hiyo.


Mtuhumiwa huyo ameiomba mahakama kumpunguzia adhabu kutokana na kuwa kwake yeye hilo ni kosa la Kwanza na pia alisema ana familia inayomtegemea hivyo aliiomba mahakama izingatie utetezi wake huo.


Jaji Mwenempazi amesema kuwa kwa kuzingatia kifungu cha sheria namba 196 hadi namba 197 kanuni ya makosa ya adhabu mahakama imemuhukumu mshitakiwa kunyongwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post