MADIWANI WACHARUKA KATIKA KATIKA YA UMEME SHINYANGA...MENEJA TANESCO ATAJA SABABU



Madiwani Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha baraza.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, wametaka ufafanuzi kwa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Shinyanga, kutoa ufafanuzi juu ya kukatika katika kwa umeme mara kwa mara katika Manispaa hiyo.
 
Wamesema tatizo la kukatika kwa umeme limekuwa kero katika Manispaa hiyo, hali ambayo imekuwa ikisababisha wananchi kushindwa kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Wamebainisha hayo leo Oktoba 28, 2022 kwenye Baraza la kawaida la Madiwani la Robo ya kwanza mwaka wa fedha (2022/2023)wakati wa uwasilishwaji wa taarifa za utekelezaji wa miradi kutoka taasisi mbalimbali za Serikali.

Mmoja wa Madiwani hao Zuhura Waziri ambaye ni diwani wa vitimaalum, amesema tatizo la kukatika kwa umeme katika Manispaa ya Shinyanga limekuwa kero, pamoja na kushusha heshima ya viongozi kwa wananchi kuwa wameshindwa kuwajibika kutatua tatizo hilo.

“Naiomba Serikali iangalie utaratibu kuwepo na Shirika mbadala ambalo litaisaidia Tanesco katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi, kama zilivyo taasisi zingine za maji na barabara, ambapo kuna Ruwasa na Shuwasa, Tarura na Tanroads, lakini Tanesco iko peke yake ndiyo maana huduma zao siyo nzuri,”amesema Waziri.

Naye Diwani wa Kizumbi Rubeni Kitinya, ameliomba Shirika hilo kama kuna mgao wa umeme ni bora waseme ili wananchi wafahamu kuliko ilivyo hivi sasa, ambapo tatizo la kukatika kwa umeme limekuwa kubwa.

“TANESCO kama kuna mgawo wa umeme ni bora mseme ili wananchi wafahamu,ukiona huku umeme unawaka eneo jingine umeme umekatika sasa hayo matengenezo ya aina gani tuwekeni wazi tu,”amesema Kitinya.

Aidha, diwani wa viti maalum Pica Chogelo, naye aliwasilisha kilio kwa Tanesco kuwa kati ya Kata zote 17 za Manispaa ya Shinyanga, Kata ya Mwamalili ni Kata pekee ambayo haina huduma ya umeme, na kuomba watekelezewe ili wananchi wapate huduma hiyo na kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo.

Kwa upande wake Meneja wa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Shinyanga Mhandisi Grace Ntungi, ametolea ufafanuzi suala la kukatika kwa umeme kuwa linatokana na hitilafu ya miundombinu ya uzalishaji na usambazaji umeme, pamoja na matengezo ya dharura na kinga.

Amesema Shirika hilo linaendelea na juhudi mbalimbali za matengezo, ili kuhakikisha hali ya kawaida inarejea na umeme usikatike tena.

Pia katika baraza hilo la madiwani ziliwasilishwa taarifa mbalimbali za kamati ikiwamo kamati ya uchumi, afya na elimu, Kamati ya mipangao miji na mazingira, Kamati ya fedha na utawala,pamoja na taarifa ya Mkurugenzi.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye kikao cha baraza.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Getruda Gisema akizungumza kwenye baraza la madiwani.

Meneja wa Shinyanga la umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Shinyanga Mhandisi Grace Ntungi, akiwasilisha taarifa ya Shirika hilo kwenye baraza la madiwani.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko (kushoto) akiwa na Naibu Meya Ester Makune kwenye kikao cha baraza la madiwani.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha baraza.

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha baraza.

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha baraza.

Diwani wa Vitimaalum Zuhura Waziri akiwa kwenye kikao cha baraza.

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha baraza.

Diwani wa Kambarage Hassani Mwendapole akiwa kwenye kikao cha baraza.

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha baraza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments