MLIPUKO MGODINI WAUA WATU 41


Takriban watu 41 wamethibitishwa kufariki baada ya mlipuko kutokea kwenye mgodi wa makaa katika mji wa Amasra kaskazini mwa Uturuki, katika jimbo la pwani la Bartin kwenye Black Sea, maafisa wamesema Jumamosi jioni.


Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki, Suleyman Soylu alilitembea eneo hilo na kutoa habari za ziada kuhusu tukio hilo.


“Tuliondoa mabaki ya watu 40 kwenye migodi yetu, majeruhi wetu tuliwapeleka hospitali. Watu 11 waliojeruhiwa walipatiwa matibabu katika hospitali kadhaa. Kati ya wachimbaji 110, wachimbaji 58 ama waliokolewa wakati juhudi kubwa za kuwatafuta na kuwaokoa waathirika kazi iliyofanywa na timu maalum, au wengine walitoka wenyewe kwenye migodi.”


Uchunguzi kuhusiana na sababu za ajali hiyo tayari zilikuwa zinaendelea, mamlaka zimesema, lakini tathminiya awali iliashiria kwamba mlipuko huo ulisababishwa na gesi maalum ambayo inatumika kwenye mgodi na inaweza kulipuka.


Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan aliitembelea Amasra siku ya Jumamosi na kuthibitisha idadi ya waliofariki wakati akiwa katika ziara kwenye eneo la tukio.

Kiasi cha wachimbaji mkaa 300 waliuawa katika mlipuko mwaka 2014 katika mji wa magharibi wa Soma, kiasi cha kilometa 350 kutoka Istanbul. Ilikuwa ni ajali mbaya sana kuwahi kutokea katika mgodi nchini Uturuki.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post