RUWASA KISHAPU WAENDESHA YAKUTANA NA WADAU WA MAJI, DC MKUDE AWAPONGEZA KUTEKELEZA MIRADI KWA VIWANGO VINAVYOTAKIWA

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye mkutano wa Ruwasa na wadau wa maji wilayani humo.

Na Marco Maduhu, Kishapu

WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Kishapu, wamefanya Mkutano Mkuu wa nusu mwaka na wadau wa maji wilayani humo.


Mkutano huo umefanyika leo Oktoba 27,2022 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, amewapongeza Ruwasa kwa kutekeleza Miradi ya Maji yenye ubora na kiwango kinachotakiwa, na kuonekana thamani ya fedha (value for money) na kuwaondolea adha wananchi ya Matumizi ya maji machafu.

Amesema Serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa kutekelezaji Miradi hiyo ya Maji, na kuwaomba wananchi waitunze miundombinu yake, ili Miradi hiyo iwe endelevu na kuwahudumia kwa muda mrefu.

"Wilaya ya Kishapu miaka mitano iliyopita tulikuwa na shida sana ya Maji safi na salama, lakini sasa hivi Maji yapo tena kutoka Ziwa Victoria ,na Serikali itaendelea kupeleka Maji kule ambapo hayajafika, hivyo wale mlio na Maji itunzeni Miradi hiyo na iwe endelevu," amesema Mkude.

Pia amevitaka vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii (CBWSO), kuwa fedha ambazo wanazikusanya za uuzaji wa maji, wazitumie vizuri ili kuendeleza Miradi hiyo pamoja na kusoma mapato na matumizi, na siyo kuzitumia hovyo na hatimaye kusababisha miradi kufa na kuwarudisha wananchi kwenye matumizi ya maji machafu.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese, akizungumza kwenye mkutano huo, ametoa wito kwa wananchi kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake kuilinda miundombinu ya miradi ya maji, pamoja na kutoa taarifa pale wanapoona mabomba yamepasuka ili yafanyiwe matengenezo ya haraka na kutosababisha upotevu wa maji.

Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa wilaya Kishapu, Mhandisi Dickson Kamazima, amesema lengo la Mkutano huo wa RUWASA na wadau wa maji ni kujadiliana, kutathmini, pamoja na kutafuta ufumbuzi wa changamoto ambazo zinaikabili Sekta ya Maji na kuboreshwa utoaji wa huduma.

Aidha, amesema kazi ya Ruwasa ni kutekeleza miradi ya maji kwa wananchi, na kipimo cha utendaji wao kazi ni kuona miradi hiyo inakuwa endelevu na kutoa huduma kwa muda mrefu, na kuomba viongozi wa Serikali kuanzia ngazi ya chini wailinde miradi hiyo na kutohujumiwa miundombinu yake.


Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye mkutano wa Ruwasa na wadau wa maji wilayani humo.

Katibu Tawala wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese akizunngumza kwenye mkutano huo wa Ruwasa na wadau wa maji.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Anderson Mandia akizungumza kweneye mkutano huo.

Katibu wa CCM wilaya ya Kishapu Peter Mashenji akizungumza kwenye mkutano huo.

Meneja wa Ruwasa wilayani Kishapu Mhandisi Dickson Kamazima akizungumza kwneye mkutano huo.

Wadau wa maji wilayani Kishapu wakiwa kwenye mkutano na Ruwasa.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post