DC MBONEKO AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI SEKONDARI MAZINGE MAADHIMISHO SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja na wanafunzi wa kike Shule ya Sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga mara baada ya kuwapatia taulo za kike kwa ajili ya kujistiri wakiwa katika siku za hedhi.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WANAFUNZI wa kike Shule ya Sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga, wamepewa taulo za kike na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, ambazo zimetolewa na Flaviana Matata Foundation kwa ajili ya kuwastiri wakiwa katika siku za hedhi wanafunzi hao wasikose vipindi vya masomo wanapokuwa katika siku zao.

Taulo za kike zimetolewa leo Oktoba 11, 2022 shuleni hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mtoto wa kike duniani, yenye kauli mbiu isemayo 'Haki zetu ndiyo kesho yetu'.

Akizungumza kwenye hafla hiyo,  Mboneko amemshukuru Flaviana Matata kwa kuiunga mkono Serikali katika masuala ya elimu, na kuamua kutoa Taulo za kike boksi 50 kwa wanafunzi wa kike shule ya Sekondari Mazinge, pamoja na kuahidi kujenga matundu ya choo 30.

Amesema upatikanaji wa taulo za kike kwa wanafunzi ni msaada mkubwa kwao katika kufanya vizuri kitaaluma kwa sababu hawatakosa vipindi vya masomo bali watahudhuria vyote, na kutoa wito kwa wanafunzi wafanye vizuri kitaaluma na kupata ufaulu mzuri.

“Leo ni siku ya maadhimisho ya mtoto wa kike duniani, na wakati nakuja hapa nilizungumza na Flaviana Matata na ameahidi katika Shule hii ya Mazinge atajenga matundu 30 ya choo, na ametoa taulo za kike Boksi 50,”amesema Mboneko.

“Taulo hizi za kike tutawagawia wanafunzi wote wa kike 433 kuanzia kidato cha kwanza hadi nne, pamoja na walimu wa kike, lengo hatutaki utoro wala mkose vipindi vya masomo sababu ya ukosefu wa taulo za kike,”ameongeza.

Pia Mboneko ameziagiza halmashauri kuhakikisha wanazitengea fedha shule zote ili wawe na taulo za kike za dharura, ili siku mwanafunzi akiingia katika siku zake akiwa shuleni apewe huduma hiyo haraka, na kutorudi nyumbani na kusababisha kukosa vipindi vya masomo.

Aidha, amewataka maofisa elimu na walimu walezi kutoa elimu ya Magauni Manne kwa wanafunzi, ili wapate kusoma na kutimiza ndoto zao, ambapo gauni la kwanza ni kuvaa sare za shule, la pili Joho la Mahafali, la tatu gauni la harusi, la nne gauni la uzazi, na wasiruke mtiririko huo bali waufuate na kutimiza malengo yao.

Katika hatua nyingine amewataka Wakuu wa Shule waendelee kutoa mazoezi ya mitihani kwa wanafunzi kila wiki, pamoja na kujifunza mbinu za ufundishaji, ili wanafunzi wote wawe vizuri kimasomo na kufaulu.

Amewataka pia wanafunzi wasome kwa bidii na kufaulu masomo yao, ambapo Serikali imeendelea kuwajengea miundo mbinu imara ya Shule, na mwaka huu Rais Samia ameshatoa tena fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za Sekondari.

Nao wanafunzi wa kike wa shule hiyo ya Sekondari Mazinge, wameshukuru kupewa taulo hizo za kike, huku wakiahidi kufanya vizuri kwenye masomo yao na kupata ufaulu mzuri.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Mazinge James Msimba, amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 854, wavulana 421 na wasichana 433 ambao wote wamepewa taulo za kike.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani katika shule ya Sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga, pamoja na ugawaji wa taulo za kike.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani katika shule ya Sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga,pamoja na ugawaji wa taulo za kike.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani katika shule ya Sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga, pamoja na ugawaji wa taulo za kike.

Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga Sifa Amoni akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya mtoto wa kike katika shule ya Sekondari Mazinge pamoja na ugawaji wa taulo za kike.

Diwani wa Ndembezi Victor Mmanywa akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa kike duniani katika shule ya Sekondari Mazinge na ugawaji wa taulo za kike.

Afisa elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga Lucas Mzungu akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa kike duniani, pamoja na ugawaji wa taulo za kike.

Mkuu wa shule ya Sekondari Mazinge James Msimba akizungumza kwenye maadhimisho hayo na ugawaji wa taulo za kike.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kulia) akizungumza katika Shule ya Sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga kabla ya kuanza kugawa taulo za kike.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kulia) akiandaa taulo za kike kwa ajili ya kuzigawa kwa wanafunzi wa kike katika shule ya Sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga.

Maandalizi ya kugawa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Mazinge yakiendelea.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akigawa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Mazingine Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kujistiri na hedhi.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiendelea na zoezi la kugawa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga.

Zoezi la ugawaji taulo za kike likiendelea.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (wapili kushoto)akigawa taulo za kike kwa walimu wa kike katika shule ya Sekondari Mazinge.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja na wanafunzi wa kike Shule ya Sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga mara baada ya kuwapatia taulo za kike kwa ajili ya kujistiri na hedhi.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mazinge wakiwa kwenye maadhimisho ya mtoto wa kike duniani, huku wakiwa wameshika taulo za kike.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga.

Muonekano wa boksi za taulo za kike.

Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwasili katika shule ya Sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani na ugawaji taulo za kike.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja na wanafunzi wa kike Shule ya Sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga mara baada ya kuwapatia taulo za kike kwa ajili ya kujistiri na hedhi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments