NGELELA ANG'AA TENA UENYEKITI CCM WILAYA SHINYANGA VIJIJINI, MAKOMBE ATOBOA MJINI


Mwenyekiti Mpya wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Magile Anold Makombe akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi.
Awali kabla ya uchaguzi bwana Magile Anold Makombe (wa kwanza kulia) akiwa na wagombea wenzake wa nafasi ya Uenyekiti CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, (katikati) Pendo John Sawa na (kushoto) ni Mokhe Warioba Nassor.
Awali Mshindi wa kiti cha Uenyekiti CCM wilaya ya Shinyanga vijijini Edward Ngelela (kushoto) akitetea kiti chake akiwa na Mgombea mwezake (wapili kutoka kulia) ni Mwenzetu Mgeja, ambapo nafasi hiyo waligombea wawili tu mara baada ya wagombea wengine wawili kujitoa.Na Marco Maduhu, SHINYANGA

CHAMA cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kimepata Mwenyekiti Mpya wa Chama hicho bwana Magile Anold Makombe ,baada ya kuwashinda wagombea wenzake wawili ,Mokhe Warioba Nassor na Pendo John Sawa.
Uchaguzi huo umefanyika jana Oktoba Mosi 2022 katika ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa wa Shinyanga.

Akitangaza matokeo hayo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM mkoa wa Shinyanga Msanii Richard, amesema kura zilizopigwa ni 515 iliyoharibika Moja na kura halali ni 514, ambapo bwana Magile Anold Makombe amepata kura 296, Mokhe Warioba Nassor kura 144 na Pendo John Sawa kura 74.

Amewatangaza wajumbe wengine walioshinda uwakilishi wa nafasi mbalimbali, kuwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa washindi ni watatu, ambao ni Jasinta Mboneko ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bundala Said na Masunga Otto.

Kundi la vijana washindi wanne ambao ni Chambulilo Hatibu, Dotto Joshua, Husna Seif, na Mbundi Yusuph.

Kundi la wazazi washindi wawili ambao Katambi Yusuph, na Bulugu Joseph.

Halmashauri kuu wilaya kundi la akina mama washindi Wanne, ambao ni Rabi Athumani, Suzy Luhende, Jakline Isalo, na Masawe Emmanuel.

Mkutano Mkuu CCM Mkoa washindi wawili ambao ni Ally Abdallah na Gabo Nduye.

Pia kwa upande wa CCM wilaya ya Shinyanga vijijini aliyeshinda nafasi ya Uenyekiti ni Edward Ngelela ambaye alikuwa akitetea kiti chake

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post