MIGUNA AREJEA KENYA BAADA YA KUFUKUZWA NA SERIKALIWakili Miguna Miguna, ambaye alifurushwa kutoka nchini Kenya tangu mwaka 2018, amewasili jijini Nairobi.

Dkt Miguna amewasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Kenyatta kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya.

Alipowasili uwanja wa ndege, Miguna Miguna alizungumza na vyombo vya habari na kushukuru jinsi alivyokaribishwa na wote waliosimama naye kama vile mahakama.


”Namshukuru Mheshimiwa Rais, Naibu rais na utawala wake na kila mmoja ambaye ameweka kila juhudi kuhakikisha kwamba haki zangu zimelindwa na haki za mkenya mwingine yeyote yule.”


Pia aliongeza kwamba kilichomtokea hakitakiwi kumtokea mwengine yeyote yule.

Dkt Miguna Miguna alifurushwa nchini kufuatia jukumu lake katika kuapishwa kwa kinara wa upinzani Raila Odinga kama rais wa wananchi mnamo Januari 2018.


Alishtakiwa kwa makosa yanayohusiana na uhaini na majaribio yake ya kurejea Kenya, licha ya maagizo kadhaa ya mahakama yaliyotolewa kuidhinisha kurejea kwake, ambako hakukufanikiwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post