NABII MKUU DKT. GEORDAVIE AWAPONGEZA WANARIADHA ZAIIDI YA 500 WALIOSHIRIKI NGURUMO YA UPAKO MATEMBEZI MARATHON



Na Woinde Shizza ARUSHA


Wanariadha zaidi ya 500 kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha wamefanikiwa kushiriki katika mbio za riadha zijulikanazo kama Ngurumo ya upako matembezi marathon.


Mbio hizo ambazo zimefanyika jijini Arusha juzi ambapo washindi wa mbio hizo wameweza kupatiwa zawadi mbalimbali kama fedha taslimu pamoja na medali


Akiongea mara baada ya kuhutimisha mbio hizo mratibu wa mbio hizo Mchungaji Daudi Mashimo alisema kuwa wanafanya marathoni hizo kwa upendo mkubwa sana 


Mashimo alisema kuwa wanariadha wamekimbia kilomita 10 na walianzia katika maeno ya Gymkhana kuzunguka katikati ya Viunga vya jiji la Arusha na kuhitimisha Gymkhana.


Alisema kuwa mbio hizo ni msaada mkubwa sana kwa afya kwa kuwa riadha ni mojawapo ya mazoezi ambayo yanafanya mwili uweze kuwa imara.


"Pamoja na kuwa sisi tunahubirk injili bado tuna sehemu kubwa sana ya kuweza kuhimiza michezo kama huu ambapo michezo bado inatakiwa iweze kuendeleza kufanywa ,"alisema.


Katika hatua nyingine alisema kuwa kwa Sasa wanatarajia kufanya mbio nyingine katika mkoa wa Mbeya ambapo napo huenda wanariadha zaidi ya 500 wakashiriki katika marathoni hiyo ijulikanayo kama Ngurumo ya upako marathon.


Aliongeza kuwa washindi katika mchuano huo wa riadha watapata zawadi kama fedha taslimu,lakini hata medali lengo likiwa ni kuwafanya watu wawe pamoja na kuhimiza mazoezi.


Hata hivyo aliwataka viongozi wa dini kuhakikisha kuwa wanaoha mfano wa mbio hizo za Ngurumo ya upako marathon kwa kuaanda michezo pamoja na matamasha mbalimbali ya michezo.


Naye Nabii mkuu wa huduma ya Ngurumo ya upako  GeorDavie aliwapongeza sana wanariadha ambao wameshiriki huku akiwapatia zawadi kama hamasa ya kuendelea kufanya vema zaidi.


"Nawapongeza sana sana wote ambao mmeweza kushiriki na ninawashika mkono washindi wote,Huku nikiwasisitiza kuwa michezo ni mizuri kwa afya ,"aliongeza.


Alimtaka mratibu wa mbio hizo kuendelea na hamasa ya kuandaa mbio hizo sehemu nyingine kwa ajili kuimarisha mwili.


Nao washiriki wa mbio hizo walisema kuwa wanamshukuru sana Nabii mkuu,kwa kuwapa zawadi za mshitukizo(surprise)ya kiasi Cha laki moja kwa kila mshindi,ni ishara nzuri na inawajengea njia na mbinu za kujiamini zaidi.



 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments