

Gewoma Goldmine Company Limited ni kampuni ya wachimba madini mkoani Geita ambayo hivi Sasa imewekeza kwenye uchimbaji wa madini ya viwanda aina ya Kaolin.
Madini ya Kaolin yanatumika kutengeneza bidhaa mbalimbali za viwandani ikiwemo saruji, vyombo vya udongo, vigae, rangi za nyumba, dawa, mbolea dawa za mswaki.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni hiyo Hellen Maduhu amesema anayo furaha kushiriki katika maonyesho ya tano ya teknolojia ya madini na kuwa Kampuni pekee iliyoweza kuonyesha madini aina ya Kaolin yanayotumika katika uzalishaji wa bidhaa za viwandani.
Kutokana na uwepo wa utajiri mwingi wa madini aina ya Kaolin Kanda ya ziwa ambayo kampuni hiyo imeyabaini, Kampuni Sasa inakaribisha wawekezaji mbalimbali wa viwanda vya saruji, vigae na malighafi nyinginezo ili kuwekeza
Social Plugin