TANZANIA,VENEZUELA KUSHIRIKIANA KWENYE ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Waziri wa elimu, sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda 

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda akiwa kwenye mazungumzo na Naibu Waziri wa Venezuela Yuri Pimentel anayeshughulikia maswala ya Afrika jana Septemba 5, 2022.


Na Mwandishi wetu,DAR ES SALAAM 

WAZIRI Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Awdolf Mkenda jana tarehe 5 Septemba 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Venezuela Mhe Yuri Pimentel anayeshughulikia maswala ya Afrika.


Mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam na kujadiliana kwa kina kuhusu mambo mbalimbali ya ushirikiano kwenye elimu, sayansi na teknolojia.


Mara baada ya mazungumzo hayo Waziri Mkenda alishudhudia utiaji saini ya makubaliano kati ya Tanzania na Venezuela kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu, sayansi na teknolojia uliofanywa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Balozi Liberata Mulamula na Naibu Waziri huyo wa Venezuela Mhe Yuri Pimentel anayeshughulikia maswala ya Afrika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post