SEPESHA RUSHWA MARATHON KUTIKISA DODOMA

 
Mwenyekiti wa Sauti ya wapinga Rushwa Mkoa wa Dodoma Haruna Kitenge akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu Sepesha rushwa marathon inayo tarajiwa kufanyika Desemb 11,2022 Dodoma. 

Na Dotto Kwilasa,DODOMA


JUMLA ya washiriki 2000 wanatarajia kushiriki mashindano ya Sepesha Rushwa Marathon yanayotarajia  kufanyika Desemba 11 mwaka huu Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Sauti ya wapinga Rushwa Mkoa wa Dodoma,ambaye ndio mratibu wa mbio hizo,Haruna Kitenge alisema washiriki hao ni wanafunzi wa shule za msingi,sekondari na vyuo,watumishi wa serikali na taasisi mbalimbali pamoja na wakimbiaji mbalimbali.

Kitenge alisema mbio watakazokimbia ni Km 21,10,5 na 3 lengo la mashindano hayo ni kuwaelewesha vijana kuhusu madhara ya rushwa pamoja na kutafuta fedha kwa ajili ya  kuendeleza kampeni ya Sepesha Rushwa katika Jiji la Arusha.

Hata hivyo Kitenge aziomba kampuni,taasisi binafsi na mashirika kujitokeza kudhamini mbio hizo.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dodoma,Robert Mabonye aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kushiriki mbio hizo.

Alisema hiyo ni fursa kwao kwani matukio kama hayo yamekuwa ni nadra kufanyika mkoani humo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post