RAIS SAMIA KATIKA BANDA LA TIC MKUTANO WA WANAWAKE WAFANYABIASHARA AFRIKA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) John Mnali (wa kwanza kulia) akielezea namna kituo hicho kinavyohamasisha Uwekezaji kwa wanawake na vijana sambamba na kutoa ushirikiano kwa makundi hayo wakati wanapotaka kufanya shughuli za uwekezaji.

Rais Samia alitembelea katika Banda la Taasisi hiyo mapema leo asubuhi kabla ya kufungua rasmi Mkutano wa Wanawake na Vijana ulioandaliwa na Sekretarieti ya eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) unaofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 12 hadi 14,2022 katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. (wa pili kulia) ni Afisa Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano TIC, Pendo Gondwe.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Maofisa wa TIC mara baada ya kupata maelezo katika Banda hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post