MKE WA MTU MWENYE UMRI WA MIAKA 15 AUMIZWA VIBAYA NA MMEWE AKISHIRIKIANA NA RAFIKI KISA KAMWAGA DAWA YA MBUZI

 

Mesoni Kashiro (15) Mkazi wa Kijiji Cha Gelailumbwa kata ya Gelailumbwa Tarafa ya Ketumbeine wilayani Longido Mkoani Arusha ameshambuliwa na mume wake Namendea Lesiria kwa kushirikiana na Rafiki yake ambaye jina halijafahamika kwa kosa la kumwaga dawa ya mfugo aina ya mbuzi.

"Huu ni ukatili kabisa kwanza ameolewa akiwa na umri mdogo ,wamempiga wakiwa wamemfunga kamba na kumtundika kwenye miti" alidai Chisunga

Hayo yameelezwa na Ofisa Ustawi wa Jamii wilayani hapa Atunagile Chisunga akieleza kuwa watuhumiwa wapo kituo Cha Polisi Longido na hapo kesho wanatarajia kufikishwa mahakamani huku akisistiza mama huyo yupo kituo Cha afya Longido akiendelea kupatiwa  matibabu zaidi.

Chanzo - Msumba News blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post