DMI YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA BAHARI DUNIANI KILWA MKOANI LINDI

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Atupele Mwakibete akizungumza na wananchi katika hotuba ya uzinduzi wa wiki ya Bahari duniani iliyofanyika kitaifa katika wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Mwakibete America rai Kwa watumiaji wa usafiri wa bahari, mito na maziwa kuzingatia utunzaji na uhifadhi wa mazingira ili yaweze kuwatunza. Mwakilishi wa mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam, Kapt. Mohamed Kauli akisalimiana na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe Atupele Mwakibete katika maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliyofanyika Kilwa mkoani Lindi Mhandisi Ibrahim Mpapi akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe Atupele Mwakibete kuhusiana na mchango wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam katika sekta ya Bahari.

**********************

CHUO cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimeshiriki katika maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani Kilwa mkoani Lindi ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya mwaka 2022 " Teknolojia mpya Kwa uchukuzi wa kulinda mazingira, inaonesha hitaji la kuunga mkono uhifadhi wa mazingira katika shughuli za usafiri na usafirishaji katika bahari, maziwa na mito duniani".

Maadhimisbo haya yatafanyika Kwa muda wa siku nne kuanzia tarehe 26 - 29/09/2022 ambapo shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwa ni pamoja na kutembelea Mialo ili kukutana na watumiaji wa vyombo vidogo vya usafiri na usafirishaji majini kwa lengo la kutoa elimu, kufanya elimu mashuleni na kutoa elimu ya usafiri na usafirishaji majini pamoja na maonesho katika mabanda maalum yaliyoandaliwa Kwa ajili ya kutoa elimu ya usafiri na matumizi sahihi ya Bahari.

Akizungumza katika maadhimisho hayo leo mkoani Lindi, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Atupele Mwakibete amesema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 inatarajia kununua meli nane za uvuvi za kisasa ambazo zitagawiwa Tanzania Bara nne na Zanzibar nne ambazo zitakuwa chachu ya kuinua uchumi wa bluu.

Pia amesema Serikali inatarajia kujenga bandari ya uvuvi ya kisasa katika wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi ambayo itaongeza fursa za kuinua uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja.

Aidha Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe Atupele Mwakibete alitembelea mabanda mbalimbali kujionea shughuli zinazofanywa na wadau wa Bahari

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments