POLISI YAUA KWA RISASI 'PANYA ROAD' SITA DAR...WANASWA NA MAPANGA


Na Andrew Chale - Dar es salaam

JESHI la Polisi Kanda maalum Dar es Salaam, limefanikiwa kuwaua Wahalifu sita maarufu kama Panya Road waliokuwa wakielekea eneo la Goba kufanya uhalifu jana Septemba 17,2022

Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana huu, Kamanda wa Polisi wa Kanda maalum, Jumanne Muliro amesema baada ya taarifa fiche kutoka kwa Wananchi wema, walibaini kuwa, wahalifu hao wakiwa Kwenye Noah, kutoka eneo la Mabibo kuelekea Goba kufanya uhalifu, na ndipo walipowakamatia eneo la Makongo Area 4.

"Tuliweka mtego, na tuliwasimamisha eneo la Makongo, na walikuwemo watuhumiwa 9 wa ujambazi wakiwa na vifaa vya jadi maarufu panya Road, walitoka na mapanga ndani ya Noah hiyo kwa lengo la kutoroka chini ya Ulinzi,"alisema.

"Askari waliwatadharisha na kujihami, na kupiga risasi juu, na kutaka Kila njia wasitoroke, lakini katika purukushani hizo Sita walijeruhiwa vibaya na watatu wakatoroka, Wahalifu hao sita, walipeleka hospitali lakini wakapoteza maisha, "alisema.

Kamanda Jumanne Muliro alisema eneo la tukio waliweza kukamata mapanga Tisa, na kisu kimoja na dhana za kuvunjia katika matukio mbalimbali.

"Uchunguzi wa awali, kwa watuhumiwa hao umebaini kuwa miongoni ni viongozi wa makundi hayo ya kutumia silaha, na wapo waliopata kuhukumiwa na kutoka Kisheria.

Aidha, Kamanda Jumanne Muliro amewataja waliotambulika kati ya waliopoteza maisha kuwa, Salum Juma Maarufu kama Babu Salum umri kati ya miaka (20-27) mkazi wa Mbagala.

Pia mwingine, ni Kharifa Kharifa mkazi wa Buguruni ambaye nae inaonesha aliwahi kukamatwa kwa makosa ya uhalifu wa kutumia mapanga Dar es Salaam.

Pia amebainisha katika Upelelezi umebaini kuwa, vinara hao walishiriki kwenye tukio la Kawe, na eneo la Buguruni kwa kuiba na kuua.

Kamanda Jumanne Muliro amesema, Jeshi la Polisi linaendelea kutekeleza kwa haraka agizo lililotolewa na Mkuu wa Jeshi hilo la kuwashughulikia wahalifu nchini.

"....Jeshi linawapongeza Wananchi kwa kutoa taarifa za usalama kwa watu wanaopanga ama kutekeleza vitendo vya uhalifu. Jeshi la Polisi linaendelea kuwatahadharisha kuacha mara Moja matukio ya uhalifu, na watakaokaidi wataendelea kuwakamata na kuwachukulia hatua.
 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post