MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA WAJADILI TAARIFA YA HESABU ZA MWISHO MWAKA WA FEDHA 2021/2022

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune akiongoza kikao cha Baraza la Madiwani.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wamejadili taarifa ya hesabu za mwisho za halmashauri kwa mwaka wa fedha (2021-2022) unaoishia June 30.

 

Kikao hicho cha Baraza la Madiwani kimefanyika leo Septemba 27, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Madiwani wakijadili taarifa hiyo, wameitaka halmashauri kulipa madeni ambayo wanadaiwa na watumishi, pamoja na wazabuni ambao hutoa huduma mbalimbali kwenye halmashauri hiyo.

Diwani wa kata ya Masekelo Peter Koliba na Ezekiel Sabo wa Ibinzamata, wamesema si vyema watumishi wakaendelea kudai madeni yao pamoja na wazabuni kwa muda mrefu, bali uangaliwe utaratibu na kulipwa madeni hayo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, naye amesisitiza suala hilo la malipo kwa watumishi na wazabuni, na kuagiza kila idara iangalie madeni ambayo wanadaiwa na watumishi wake na kuanza kuyapunguza.

Aidha, amewasihi madiwani pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, waendelee na kasi ya ukusanyaji mapato ya ndani kama ilivyo sasa na wasibweteke, pamoja na kutumia lugha nzuri wakati wa kukusanya mapato hayo.

Pia Mboneko amesisitiza suala la usimamizi wa fedha za miradi ya maendeleo, ili miradi hiyo itekelezwa kwa kiwango bora.

Katika hatua nyingine, Mboneko amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha Sh. Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na Wodi katika kituo cha afya Kambarage ili kuboresha utaoaji wa huduma za matibabu kwa wananchi.

Akizungumzia suala la chakula, amewataka wananchi kuhifadhi vyakula na kutoviuza hovyo, wala kufanya sherehe za kutumia vyakula vingi ili wawe na akiba ya chukula kwenye Kaya zao, kutokana na hali ya hewa siyo nzuri ya upatikanaji wa mvua za kutosha.

Amegusia Pia suala la wanafunzi ambao watafanya Mtihani wa kuhitimu darasa la Saba Oktoba mwaka huu, kuwa watoto wote wafanye mtihani huo na hakuna hata mmoja kuozeshwa.

Kaimu Mweka hazina wa Manispaa ya Shinyanga Marco Masele, akisoma taarifa hiyo ametaja madeni ambayo wanadaiwa na watumishi, kuwa ni Sh.milioni 669.7 na fedha za Wazabuni Sh. Milioni 1.8, huku wakikusanya mapato ya ndani Sh. Bilioni 5.061.


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga.

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Rajab Masanche akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Kaimu Mweka hazina wa Manispaa ya Shinyanga Marco Masele, akisoma taarifa ya hesabu za mwisho za halmashauri kwa mwaka wa fedha 2021/2022 unaoishia June 30.

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.

Kikao cha Baraza kikiendelea.

Kikao cha Baraza kikiendelea.

Kikao cha Baraza kikiendelea.

Kikao cha Baraza kikiendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments