MBUNGE SALOME MAKAMBA ATOA MSAADA WA MAGODORO, VITANDA KWA WATOTO YATIMA SHINYANGA


Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Shinyanga Salome Makamba, (kulia) akikabidhi Magodoro 10 katika kituo cha kulelea watoto Yatima Mjini Shinyanga, (kushoto) ni Mwanzilishi wa kituo hicho Elias Fue.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MBUNGE wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Salome Makamba, ametoa msaada wa Magodoro na Vitanda katika kituo cha watoto yatima (Teenagers Foundation Tanzania Orphanage Centre) kilichopo Majengo Mapya Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.

Makamba ametoa msaada huo leo Septemba 26, 2022, kwa lengo la kuunga mkono juhudi za wadau za kusaidia watoto wenye uhitaji, ili waishi katika mazingira mazuri pamoja na kusoma kwa bidii na kutimiza ndoto zao.

Amesema kusaidia wenye uhitaji ni kufungua milango ya neema na kupata thawabu kwa mwenyezi Mungu, na kuwataka wadau mbalimbali wa maendeleo na wenye nafasi, kujenga utamaduni wa kusaidia watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu.

“Nimeguswa na kituo hiki cha kulelea watoto Yatima hapa Majengo Mapya, hivyo nikaona ni vyema na mimi nitoe mchango wangu wa kuwasaidia watoto hawa kuwapatia vitanda vitano (double decker bed) pamoja na Magodoro 10, ili walale sehemu nzuri,”amesema Makamba.

“Kwa nafasi yangu niliyonayo nitaendelea kuwatafutia wadau mbalimbali ili kuendelea kuwatatulia changamoto ambazo bado zinawakabili watoto hawa, ikiwamo sehemu nzuri ya kujisomea, kuwapatia vitabu, ili wasome na kutimiza ndoto zao,”ameongeza.

Nao watoto hao Yatima akiwamo Clemensia Clement ambaye anasoma kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari Ngokolo, amemshukuru Mbunge huyo kwa msaada wake huo, ambao umewaondolea adha ya kulala chini , huku wakimuahidi kufanya vizuri katika masomo yao.

Kwa upande wake Mwanzilishi wa kituo hicho cha watoto Yatima Elias Fue, amemshukuru Makamba kwa kuitikia maombi yao, na kuamua kuwaunga mkono katika kutatua baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili, na kubainisha kuwa kituo hicho kinajumla ya watoto 15.

Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Shinyanga Salome Makamba akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi Magodoro 10 katika kituo cha watoto Yatima, ambapo vitanda vitano vyenyewe bado vipo kwa fundi.
Mwanzilishi wa kituo cha kulea watoto Yatima Elias Fue, akitoa shukrani ya msaada huo wa Magodoro 10 na vitanda Vitano ambavyo vinamaliziwa kuchongwa kwa fundi.

Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Salome Makamba, (kulia) akikabidhi Magodoro 10 katika kituo cha kulea watoto Yatima, (kushoto) ni Mwazilishi wa kituo hicho Elias Fue.

Zoezi la kukabidhi Magodor0 likiendelea.

Mwanzilishi wa kituo cha kulea watoto Yatima Elias Fue, (kushoto) akimshukuru Mbunge Salome Makamba kwa msaada huo.
Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Salome Makamba, (kulia) akifurahia jambo na Mwanzilishi wa kituo cha kulea watoto Yatima Elias Fue, mara baada ya kumaliza kutoa msaada wa Magodoro kituoni hapo.

Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Shinyanga Salome Makamba, akifurahia jambo na baadhi ya watoto Yatima ambao wanalelewa kwenye kituo hicho.

Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Salome Makamba, akifurahia jambo na baadhi ya watoto Yatima ambao wanalelewa kwenye kituo hicho.

Muonekano wa kituo cha kulea watoto Yatima.

Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Salome Makamba, akifurahia jambo na baadhi ya watoto Yatima ambao wanalelewa kwenye kituo hicho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post