WALIMU WAPIGWA MARUFUKU KUKIMBILIA MJINI


Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka ametoa zuio kwa walimu wa ajira mpya kuhama kutoka maeneo ya vijijini waliopangiwa kazi na serikali kwani kwa kufanya hivyo kumekuwa kikiathiri kiwango cha ukuaji wa elimu hususani maeneo ya vijijini.

Mkuu wa Mkoa amesema hayo wakati akikabidhi vitabu vya mwongozo wa namna ya ufundishaji ambapo mkuu wa mkoa amesema kuwa kumekuwa na tabia ya walimu kupewa ajira na serikali na baadaye kuanza kuomba kuhamia mijini kwa sababu ambazo hazina mashiko

Katika Kikao hicho pia mkuu wa mkoa amesikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi na kuahidi kuzifanyia ufumbuzi.

Afisa elimu mkoa wa Njombe mwalimu Neras Aron Mulungu amesema kuwa wananchi mkoani Njombe wamefanya kazi kubwa kujenga nyumba za walimu huku akisema tabia ya walimu kukimbilia mijini inatokana na hulka ya mtu binafsi huku akisema kwa sasa huduma zote zilizopo mjini kama umeme zimefikishwa mpaka vijijini.

CHANZO-EATV




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments