MCHUNGAJI MGOGO AWACHANA VIJANA WACHANGA WANAOLELEWA NA MASHUGA MAMI....."UNAKULA MALI YA BABU YAKO?"Mtumishi wa Mungu Mtanzania Mchungaji Daniel Mgogo amewataka vijana wachanga kuchumbiana na wasichana wa wenzao wa umri wao.

Akizungumza wakati wa ibada ya hivi majuzi kanisani, pasta huyo alibainisha kwamba idadi ya vijana wa kiume wanaochumbiana na mashuga mami inatisha.

Mhubiri huyo alisuta vijana ambao wajiingiza katika mapenzi na wanawake wanaowazidi kwa umri.

 Mgogo alisema ni fedheha kwa vijana wa kiume kuchumbiana na wanawake wakubwa huku akieleza kuwa ni kupoteza muda kwani hawawezi kupata watoto pamoja.

"Kijana mbichi anajihusisha na mashuga mami. Baba zake walijihusisha na wamama wakubwa, na yeye pia sasa anafuata mkondo huo huo. Baba zake walizaa watoto na huyu mama na wewe unafuatana na yeye, utazaa watoto na huyu ana miaka sabini. halafu mnatuambia, umri namba. 

Vijana tunategemea waoe tufenge harusi, watuletee wajukuu. Watu wanaskumana na mibibi minyanya. Na wanyanya wengi hawataki waonekane wako na mapengo, wameenda kununua meno bandia lakini sura inaonyesha wewe ni mzee.

Kweli kijana mdogo jitegemee, unataka kula mali za babu yako aliyekufa alimuacha huyu bibi?. Achana na huyo mama! Nenda tafuta size yako," Mgogo alisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post