WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WAPATIWA MAFUNZO YA POLIO

Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Shinyanga, Timoth Sosoma akizungumza wakati wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Ofisi ya Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga imetoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano ambayo inafanyika nyumba kwa nyumba kwa kuwapatia watoto matone ya chanjo.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Ijumaa Septemba 2,2022 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Shinyanga, Timoth Sosoma amesema waandishi wa habari wana nafasi kubwa ya kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu ugonjwa wa Polio, Chanjo ya Polio na kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Polio.

“Tunatambua umuhimu wa waandishi wa habari katika kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu ugonjwa Polio na kuifanya jamii kuwa na mtazamo chanya juu ya chanjo ya polio lengo likiwa ni kumkinga mtoto dhidi ya ugonjwa wa kupooza”,amesema Sosoma.

Amesema katika Kampeni ya Chanjo ya Polio awamu ya tatu iliyoanza Septemba 1,2022 na kutarajiwa kuhitimishwa Septemba 4,2022 wanatarajia kuwapatia chanjo watoto 445,681 wenye umri chini ya miaka mitano ili kuwakinga na ugonjwa wa Polio.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile amesema Chanjo ya Polio ni salama, haina madhara na wanafanya kampeni ya chanjo ya polio nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha kila mtoto anapata chanjo ya badala ya kuwasubiri kwenye vituo vya afya wapate chanjo.
Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Shinyanga, Timoth Sosoma akizungumza wakati wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Waandishi wa Habari wakiwa kwenye mafunzo kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post