ALIYESHANGILIA RAILA ODINGA KUSHINDWA URAIS AZINGULIWACliff Onrichi

CLIFF ONRICHI ameonekana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii akishangilia kwa furaha Raila Odinga kushindwa urais nchini Kenya.


Kutokana na video hiyo kusambaa, imeonekana kuwa mwajiri wake wa Kampuni ya Mabasi Transline Classic hakupendezwa na tukio hilo.


Hivyo, kampuni hiyo imetoa barua ya kuwaomba radhi watu, kwa kitendo kilichofanywa na Cliff na kubainisha kuwa tayari amechukuliwa hatua za kinidhamu.


Nanukuu hapa kilichoandikwa katika barua ya Transile Clasic

“Kwa wateja wetu wapendwa, tumefikiwa na video klipu inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii, iliyofanywa na Cliff Onrich ambaye ni mfanyakazi wa kawaida anayeishi katika ofisi zetu za kituo cha afya.

Kampuni ya Usafirishaji ya Transline Classic

Kama kampuni tunataka kujitenga na klipu hiyo na kueleza kuwa klipu hiyo ilifanywa kwa utashi wake binafsi na haiwakilishi mitazamo ya kampuni hivyo, hatua za kinidhamu zimechukuliwa dhidi yake.

Tunaomba radhi kwa kila mtu hususani kwa wateja wetu wathamini kutokana na kukasirishwa na klipu hiyo, kama kampuni tupo kwenye biashara na sio kwenye siasa, tutaendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wetu wote” mwisho wa kunukuu.


Imeandaliwa na Sanifa Khalifa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post