DC MBONEKO AKABIDHI MIKOPO YA SH. MILIONI 156.4 KWA MAKUNDI YA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU MANISPAA YA SHINYANGA

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (aliyevaa miwani) akikabidhi hundi ya Mikopo ya shilingi Milioni 156.4 iliyotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa Vikundi 11 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amekabidhi Mikopo ya shilingi Milioni 156.4 (Tsh. 156, 454,000/=) iliyotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa Vikundi 11 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali ikiwa ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashari hiyo kwa kipindi cha mwezi Aprili – Juni 2021/2022.

Mbali na kukabidhi mkopo huo wa fedha taslimu, pia Mboneko amekabidhi baadhi ya vifaa vya usafi kwa vikundi ambavyo vilipatiwa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri hiyo.

Hafla fupi ya kukabidhi mikopo hiyo imefanyika leo Jumanne Septemba 27,2022 kata ya Kitangili katika eneo la ghala la kuhifadhia mazao lililonunuliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambalo ndani yake kuna mashine ya kukoboa nafaka, visima vya maji,banda la kufugia kuku, ofisi ndogo, wanyama na mabwawa ya kufugia samaki linalosimamiwa na Muunganiko wa vikundi vitatu vya Wanawake (Ndembezi, Ibadakuli na Masekelo – NDEIMA).

Akizungumza wakati wa kukabidhi Mikopo hiyo, Mboneko amewataka wanakikundi hao kwenda kutumia mikopo kwa malengo yaliyokusudiwa na kurejesha kwa wakati ili vikundi vingine vipatiwe mkopo huo.

“Fedha hizi tunazowapa zikafanye kazi kweli kweli ili muwa mfano, nendeni mkafanye kazi kwa ushirikiano na mshikamano. Na endapo mtapata changamoto toeni taarifa. Unapopata changamoto sema”,amesema Mboneko.

“Nanyi Maafisa Maendeleo ya jamii hakikisheni mnasimamia vikundi hivi na muwape elimu namna ya kuendeleza miradi yao”,amesema Mboneko.

Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Elias Ramadhani Masumbuko amesema halmashauri hiyo itaendelea kutoa mikopo kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwani lengo ni kuwezesha wananchi wapige hatua kiuchumi.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Dkt. Jomaary Satura amesema halmashauri hiyo imenunua eneo kwa ajili ya wajasiriamali katika kata ya Kitangili ili kuwawezesha wajasiriamali kufanya shughuli zao na kuhakikisha vikundi vyote vinanufaika na mikopo inayotolewa na halmashauri.

Mwenyekiti wa Kikundi cha NDEIMA, Juliana Ndalahwa amesema kikundi hicho kilianzishwa kufuatia muunganiko wa vikundi vitatu vya wanawake ambavyo maandiko ya maombi yao ya mikopo yalikuwa yanafanana.

Mwenyekiti huyo wa NDEIMA ametumia fursa hiyo kuuomba uongozi wa wilaya ya Shinyanga na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuwasaidia kutafuta tenda za kusambaza nafaka kwenye taasisi mbalimbali huku akieleza kuwa matarajio yao mengine ni kusambaza samaki katika taasisi mbalimbali ikiwemo katika magereza.

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, John Tesha amesema kikundi cha NDEIMA wamekipatia mkopo wa Shilingi 80,454,000/= pamoja kukieleza kufanya shughuli zao ndani ya eneo hilo lililonunuliwa na Halmashauri kwa muda wa miaka mitatu.

Mbali na kikundi cha NDEIMA pia wametoa mikopo kwa vikundi vingine 10 vikiwemo vikundi vine vya watu wenye ulemavu hivyo kufanya idadi ya vikundi vilivyopewa mikopo kuwa 11 vyote vikipata mkopo wa jumla ya shilingi milioni 156.4.

“Nitumie nafasi hii kuwakumbusha wanavikundi wote wanaokopeshwa na wale waliokwishakopeshwa wakumbuke kuwa mikopo hii wanayopatiwa lazima ikatekeleze miradi iliyoombwa na siyo vinginevyo. Kutotekeleza miradi waliyoombea mikopo au kubadilisha miradi iliyoombewa mikopo ni kinyume cha sheria na watachukuliwa hatua kali. Na vikundi ambavyo havitarejesha mikopo navyo vitachukuliwa hatua za kisheria”,amesema.

Nao baadhi ya wanavikundi akiwemo Daudi Nyahiti wameishukuru Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuwapatia mikopo ambayo itawasaidia kujiinua kiuchumi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Mikopo ya shilingi Milioni 156.4 (Tsh. 156, 454,000/=) iliyotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa Vikundi 11 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Mikopo ya shilingi Milioni 156.4 (Tsh. 156, 454,000/=) iliyotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa Vikundi 11 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali.

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga John Tesha akizungumza wakati Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi Mikopo ya shilingi Milioni 156.4 (Tsh. 156, 454,000/=) iliyotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa Vikundi 11 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Dkt. Jomaary Satura akizungumza wakati Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi Mikopo ya shilingi Milioni 156.4 (Tsh. 156, 454,000/=) iliyotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa Vikundi 11 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Elias Ramadhani Masumbuko akizungumza wakati Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi Mikopo ya shilingi Milioni 156.4 (Tsh. 156, 454,000/=) iliyotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa Vikundi 11 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (aliyevaa miwani) akikabidhi hundi ya Mikopo ya shilingi Milioni 156.4 (Tsh. 156, 454,000/=) iliyotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa Vikundi 11 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (aliyevaa miwani) akikabidhi hundi ya Mikopo ya shilingi Milioni 156.4 iliyotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa Vikundi 11 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (aliyevaa miwani ) akikabidhi hundi ya Mikopo ya shilingi Milioni 156.4 iliyotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa Vikundi 11 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (aliyevaa miwani) akikabidhi hundi ya Mikopo ya shilingi Milioni 156.4 iliyotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa Vikundi 11 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (aliyevaa nguo ya njano) akikabidhi vifaa vya usafi kwa vikundi vya wajasiriamali vilivyotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (aliyevaa nguo ya njano) akitembelea mashine za kukoboa na kusaga nafaka katika eneo linalosimamiwa na kikundi cha wanawake kutoka Kata ya Ndembezi, Ibadakuli na Masekelo (NDEIMA). Katikati ni Mwenyekiti wa Kikundi cha NDEIMA, Juliana Ndalahwa.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (aliyevaa nguo ya njano) akitembelea mashine za kukoboa na kusaga nafaka katika eneo linalosimamiwa na kikundi cha wanawake kutoka Kata ya Ndembezi, Ibadakuli na Masekelo (NDEIMA).

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (aliyevaa nguo ya njano) akiangalia mabwawa ya kufugia samaki yanayosimamiwa na kikundi cha wanawake kutoka Kata ya Ndembezi, Ibadakuli na Masekelo (NDEIMA).

Mwenyekiti wa Kikundi cha NDEIMA, Juliana Ndalahwa akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Mikopo ya shilingi Milioni 156.4 (Tsh. 156, 454,000/=) iliyotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa Vikundi 11 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali.
Diwani wa kata ya Ndembezi Victor Mmanywa akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Mikopo ya shilingi Milioni 156.4 (Tsh. 156, 454,000/=) iliyotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa Vikundi 11 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali.
Diwani wa kata ya Kitangiri, Mariam Nyangaka akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Mikopo ya shilingi Milioni 156.4 (Tsh. 156, 454,000/=) iliyotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa Vikundi 11 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali.
Mnufaika wa mkopo, Daudi Nyahiti akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Mikopo ya shilingi Milioni 156.4 (Tsh. 156, 454,000/=) iliyotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa Vikundi 11 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali.
Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Viongozi mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Viongozi wa dini  (kulia) wakiwaombea Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali waliopata mikopo kutoka halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. Aliyevaa nguo ya njano ni Mkuu wa wilaya Mhe. Jasinta Mboneko.

Mkuu wa wilaya Mhe. Jasinta Mboneko akicheza muziki na Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali waliopata mikopo kutoka halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. 
Shamra shamra zikiendelea baada ya Mkuu wa wilaya Mhe. Jasinta Mboneko kukabidhi mikopo kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka kata mbalimbali iliyotolewa na halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. 

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post