Bunge la Uganda limepitisha sheria ya mtandao ikilenga watumiaji wa computer nchini humo.
Sheria hiyo tata ambayo baadhi ya wabunge wamesikika wakisema kwamba watakwenda kuipinga mahakamani itawahusu watu wanaochapisha taarifa za uongo mitandaoni,taarifa ambazo hazijathibitishwa na wahusika, pia kuchapisha taarifa za watoto bila idhini ya wazazi au walezi wao.
Wakati wabunge wa nchi hiyo wakisema ndio ili kupitisha sheria hiyo, baadhi yao walisikika wakiguna , ndipo spika wa bunge Anita Among alipowaambia watafute namna na kwenda mahakamani.
Moja ya kifungu kilichopingwa , kinahusu adhabu kwa mtu atakayerekodi sauti ama video ya mtu mwingine bila ridhaa yake ambapo atakabiliwa na faini ya shilingi za Uganda Milioni 15 (zaidi ya Tsh. Milioni 9 ) au kifungo kisichozidi miaka 10 gerezani au vyote kwa pamoja