FISI AUA MBUZI 10...AUAWA KWA KUSHAMBULIWA NA MBWA


Mbuzi waliokufa kwa kushambuliwa na Fisi
***

Mbuzi 10 wamekufa na wengine 9 kujeruhiwa baada ya kuvamiwa na kundi la Fisi usiku wa kuamkia leo Septemba 23, 2022, kwenye zizi la Masumbuko Shirungu mkazi wa Kijiji cha Itale wilayani Chato mkoani Geita na baadaye Fisi huyo aliuawa na Mbwa wa mfugaji.

Afisa Mifugo na Uvuvi wilaya Chato Dokta Elfas Msenya, ameeleza hasara iliyojitokeza kwa Mfugaji huyo.

"Mbuzi 1 kwa sasa wastani wa bei ni shilingi 90,000 zidisha mara idadi ya mifugo iliyoathirika utaona hasara ilivyokubwa", amesema Msenya.

Aidha Msenya anaelezea hatua za awali walizochukua kuhakikisha mifugo minginge haikumbani cha changamoto ya kuliwa na Fisi.

"Hatua za haraka tukizochukua kwa sasa, tumewashauri kuimarisha mabanda yao au wajenge mabanda imara bila kusahau kuimarisha ulinzi hasa nyakati za usiku lakini pia kutowafuata wanyama wakali kwenye makazi yao na waache kujenga karibu na maeneo ya mapori,".

CHANZO - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post