MGEJA : TUENDELEE KUDUMISHA AMANI YA NCHI, TUSIBAGUANE KWA RANGI, MAKABILA



Na Paul Kayanda, Shinyanga

MWENYEKITI wa Taasisi ya Mzalendo Foundation Khamisi Mgeja amewahimiza watanzania kudumisha amani upendo na mshikamano kwa kuwa ndiyo tunu ya Taifa sanjari na kufanya kazi kwa bidii ili kuchochea maendeleo nchini.

Mgeja ambaye pia alipata Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga aliyasema hayo Septemba 9 mwaka huu wakati akizungumza na wazee wenzake waliomtembelea nyumbani kwake kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusu maendeleo na mustakabali wa nchi pamoja na kutakiana kheri ya siku ya Ijumaa.

Aliwataka watanzania kuendelea kushikamana kwa kila namna na hali ya amana waendelee kuidumisha kwa kufuata demokrasia ya nchi yetu kwani kuna nchi na mataifa mengine hayaelewani.

Aidha aliwataka viongozi wa Dini na madhehebu mbalimbali nchini waendelee kuhubiri amani iliyopo ili isiharibiwe na mtu yeyote na kuongeza kuwa pia watanzania wasibaguane kwa rangi na makabila yaliyopo kwani  watanzania ni Watoto wa mama mmoja.

“Watanzania wenzangu nawaomba kwa heshima tutakiane heri, Baraka, upendo, amani na umoja wa kitaifa. Hivyo ndivyo watanzania tunachokitaka kila siku kuwepo kwa ustawi wa jamii yetu na nchi yetu kwa pamoja na umoja wetu tunaweza, KAZI IENDELEE,” alisema Mgeja.

Vile vile Mgeja alitumia fursa hiyo kuwaomba Watanzania kuendelea kumuamini na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ili achape kazi na kuwaletea maendeleo watanzania na kutufikisha sehemu inayotakiwa.

Akizungumza kwa niaba ya wazee wenzake Profesa Zacharia alimshukuru mzee Mgeja kwa kuwakaribisha nyumbani kwake huku akisisitiza kudumisha utamaduni walionao watanzania kwa na umoja na mshikamano bila kubaguana kwa kabila, dini,rangi, ukanda na jinsia kwa maslahi mapana ya nchi.



“Sisi kama wazee tunaomba utamanduni tulionao watanzania, wa umoja wa kitaifa bila kubaguana kidini, kabila, ukanda au jinsia yeyote ile tuuendeleze na kuudumisha kwa maslahi mapana ya nchi yetu, pia niseme tu tunalizishwa na amani na utulivu wa nchi yetu uliopo sasa chini ya uongozi imara na madhubuti wa mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan na tunawaomba watanzania waendelee kumuunga mkono Rais wetu kwani amani na maendeleo ni Mapacha,” alisema Profesa Zacharia.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments