CCM YAPONGEZA JITIHADA ZA RAIS SAMIA KUFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA MATUMIZI YA RASILIMALI YA GESI NCHINI


KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka amesema Chama hicho kinaipongeza Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT) kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhakikisha gesi asili inatumika kuendesha vyombo vya moto kama magari ili kupunguza gharama kubwa ya fedha inayotumika kununua mafuta nje ya nchi.

Aidha amesema Chama kinampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kiasi cha zaidi ya Sh.bilioni 100 kwa ajili ya kuiwezesha DIT kujenga vituo vya umahiri ambavyo vitakuwa chachu ya kupika watalaamu wa kada mbalimbali wakiwemo watalaamu wa kufunga mifumo ya gesi kwenye magari yanayotumia mafuta ya petroli na dizeli.

Shaka ameyasema hayo leo Agosti 29,2022 alipofanya ziara fupi ya kutembelea DIT kwa lengo la kuwapongeza na kuwatia moyo kwa kazi nzuri wanayofanya ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2020/2025 ambayo inaelezea kwa kina kuhusu uwekezaji kwenye eneo la TEHAMA.

“Kumekuwa na jitihada kubwa zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi kupitia Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia kwenye uwekezaji wa fedha nyingi za maendeleo maeneo mbalimbali .Moja ya eneo ambalo pengine hatujafika kuona namna ambavyo fedha zimewekwa na utekelezaji unaendelea ni eneo hili lililobeba teknolojia

“Nikisema teknolojia tunaamanisha mfumo mzima wa mabadiliko haya ya kidunia na hapa nazungmzia TEHAMA, leo tumepata fursa hii kuona namna ambavyo wenzetu wa DIT wanatumia utaalamu huu kubadilisha miundombinu hii ya magari kutoka kwenye mafuta kwenda kwenye gesi.

“Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kueleza kujitegemea ni kwa maana kutumia fursa vizuri kulinufaisha taifa , sasa moja ya fursa tuliyonayo ni gesi asilia ambayo imegundulika na imeanza kutumika , tunaelezwa tunayo akiba ya karibia futi trilioni 57 .5 ambayo imeifanya Tanzania kuwa nchi ya 82 duniani kwa utunzaji na umikili wa gesi asili,”amesema Shaka.

Amefafanua gesi asili imeshaanza kutumika kwa kiasi fulani kwa matumizi ya uzalishaji wa umeme lakini kwa matumizi ya viwandani

“Sasa tumekuwa tukijitanua kwenye suala zima la teknolojia , nichukue fursa hii kuwapongeza DIT kwa namna wanavyotafsiri dhana lakini kwa kusimamia na kuhakikisha kifungu cha 63 C cha Ilani ya Uchaguzi Mkuu kinatekelezeka.Bahati nzuri wanayoyatekeleza DIT sio matakwa yao ama utashi wao bali wanatekeleza Ilani ya CCM,”amesema Shaka.

Ameongeza kwa niaba ya Chama hicho wanampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo Sh.bilioni 100 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa vituo vya umahiri kwenye eneo hili.

“Kwa kiasi kikubwa kama likisimamiwa vema katika vita hii ya uchumi inayoendelea hivi sasa DIT ni kamandi muhimu katika mapambano ya uchumi.Hivyo hawa wenzetu walipewa dhamana wakifanya kazi yao vizuri matokeo yake yatakuwa makubwa na yenye tija kubwa kwenye taifa letu,”alisema Shaka.

Amesema kwanza itapunguza matumizi ya mafuta kwenye magari ,hivyo teknolojia hiyo itasaidia kupunguza matumizi ya fedha nyingi zinazotumika kununua mafuta lakini itasaidia kwenye suala la usafirishaji endapo uhamasishaji ukafanywa vizuri na wafanyabiashara wa ndani wakahamasishwa.

“Na Serikali yenyewe ikajipanga kwenye kujenga vituo vya kusambaza hiyo gesi asili. Hatua ya kwanza wanafunga mifumo kwenye magari na hatua ya pili ni kuwa na vituo kadhaa vitakavyosaidia sasa kutoa fursa pana zaidi ili wale ambao watakuwa wanatumia gesi hii kusiwe na usumbufu , tunakuwa tumepiga hatua kubwa katika dhana ya maendeleo endeleo.”

Aidha amesema teknolojia hiyo itafanya Tanzania kutumia vizuri fursa hiyo ya kidunia kama ambavyo ameeleza nchi yeti iko katika nchi 82 sio jambo dogo. “Lazima tufanye vizuri kwenye suala la taaluma na kwenye hili nadhani ndio msingi wetu mkubwa kuwa na watalaamu wa kutosha watakasimamia dhana hii.

“Tumeanza na tuna imani kwamba itakuwa na mafanikio makubwa lakini huu nadhani ni mlango mwingine wa kusaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.Naamini endapo mipango na mikakati thabiti itawekwa ni sehemu mojawapo ambayo tutaweza kuwaanda vijana wetu kutumia fursa hii ambayo imeibuliwa kuwatoa kwenye kilio cha ukosefu wa ajira ajira kwa vijana,”amesema Shaka.

Ameongeza teknolojia hiyo itatutoa kwenye utegemezi wa mafuta kama Taifa lakini si utegemezi wa mafuta tu sasa watalaamu waje na mawazo mapya na utalaamu wao utumike kushauri na maeneo mengine huko kwenye bajaji, boda boda, nako pia tukipeleka teknelojia hii na tutakuwa tumewasaidia sana vijana.

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka akipata maeelezo kutoka kwa Meneja wa Mradi wa Kuunganisha Mfumo wa Gesi Asili katika Magari (CNG), Dkt. Esebi Nyari,namna vipuri vya mifumo ya gesi inavyounganishwa kwenye magari mbalimbali,alipofanya ziara fupi ya kutembelea DIT kwa lengo la kuwapongeza na kuwatia moyo kwa kazi nzuri wanayofanya ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2020/2025 ambayo inaelezea kwa kina kuhusu uwekezaji kwenye eneo la TEHAMA.
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka akipata maeelezo kutoka kwa Meneja wa Mradi wa Kuunganisha Mfumo wa Gesi Asili katika Magari (CNG), Dkt. Esebi Nyari,namna mifumo ya gesi inavyounganishwa na kufanya kazi kwenye magari mbalimbali,alipofanya ziara fupi ya kutembelea DIT kwa lengo la kuwapongeza na kuwatia moyo kwa kazi nzuri wanayofanya ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2020/2025 ambayo inaelezea kwa kina kuhusu uwekezaji kwenye eneo la TEHAMA.

Meneja wa Mradi wa Kuunganisha Mfumo wa Gesi Asili katika Magari (CNG), Dkt. Esebi Nyari akitoa ufafanuzi kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka kuhusu mifumo ya gesi inavyounganishwa na kufanya kazi kwenye magari mbalimbali. Shaka amefanya ziara fupi ya kutembelea DIT kwa lengo la kuwapongeza na kuwatia moyo kwa kazi nzuri wanayofanya ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2020/2025 ambayo inaelezea kwa kina kuhusu uwekezaji kwenye eneo la TEHAMA.
Kikao kikendelea
MKurugenzi Mkuu wa Kampuni Tanzu ya DIT John Msumba akifafanua mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo kampuni hiyo inavvyofanya kazi ikiwemo na kutoa elimu kwa vitendo kwa Wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho

Mkuu wa Taasisi ya DIT Prof.Preksedius Ndomba akizungumza jambo mara baada ya kumkaribisha Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka aliyefanya ziara fupi ya kutembelea DIT kwa lengo la kuwapongeza na kuwatia moyo kwa kazi nzuri wanayofanya ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2020/2025 ambayo inaelezea kwa kina kuhusu uwekezaji kwenye eneo la TEHAMA. Picha na Michuzi JR.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post