SERIKALI YAMSIMAMISHA KAZI MRAJISI WA VYAMA VYA USHIRIKA TABORA KUPISHA UCHUNGUZI

-Ni maelekzo Mwenezi wa CCM kwa Wizara ya Kilimo
-Wananchi wa Kaliua, sikonge, urambo na uyui wote walilalamika kwa Mwenezi wa CCM

Cheche za Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka zimemuunguza mrajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoani Tabora Absolom Chaliga baada ya leo kusimamishwa kazi kutokana na tuhuma za kushindwa kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

Barua iliyoandikwa na Dr Benson Ndiyege ambaye ni mrajis wa vyama vya Ushirika inasema kuwa Chaliga anasimamishwa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.

”Amesimamishwa kwa mujibu wa kanuni no 37 ya kanuni za utumishi wa umma za Mwaka 2003.” Dk Ndiyege

Akiwa katika wilayani Uyui kwenye ziara yake mkoani Tabora kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, Shaka aliomba serikali kumuondoa mrajisi hiyo baada ya kupata malalamiko kila wilaya juu ya utendaji wake kazi.

“Changamoto za bwana huyu imekuwa donda sugu , tumetoka Kaliua analalamikiiwa, tumetoka Sikonge analalamikiwa, tumetoka Urambo analalamikiwa, leo tuko Uyui watu wanalia na huyu bwana. Urasimu umekuwa mkubwa sana.

“Utitiri na ukiritimba umekuwa mkubwa sana kiasi unadumaza jitihada na huko tunakotoka hajasajili vyama kwasababu kuna mawakala wanapita chini kwa chini , Mbunge kasema na mimi taarifa ninazo wako mawakala wanapita chini kwa chini kuwaambia wakulima nenda kajiunge pale. Yeye sio kazi yake , yeye sio jukumu lake la nani akajiunge ushirika gani .

“Nani ahame wapi na aende wapi, hiyo sio kazi yake hapa kuna vyama vya ushirika 18 havijasajaliwa , amesajili saba tu na hivyo saba kwasababu ya mawakala wake na inaonekana kuna mazingira ya rushwa yanatengenezwa wakati Serikali inapiga vitaa”alisema Shaka na kuongeza.

“Maelekezo yetu kwa Wizara ya Kilimo kupitia Waziri wa Kilimo amuondoe mara moja huyu Mrajisi wa vyama vya ushirika , narudia tena maelekezo kwa Waziri wa Kilimo amuondoe, kwasababu Tabora ndio inaongoza kwa kilimo cha tumbaku hivyo hawawezi kuona jitihada za Rais Samia anatokea mtu mmoja tu anazikwamisha halafu bado akaendelea kuchekewa,”alisema Shaka.





Katibu wa nec ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mfuluma, Wilaya ya Uyui mkoani Tabora akiwa katika ziara ya kukagua Uhai wa chama na Utekelezaji wa Ilani ya I chaguzi ya CCM ya 2020-2025. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post