AMUUA MKE WAKE ALIYEFUNGA NAYE NDOA MWEZI ULIOPITA



Jeshi la polisi mkoani Morogoro linamshikilia Msafiri Nasibu (31) mkazi wa kitongoji cha Maskati kata ya Tegetero Halmashauri ya Morogoro kwa tuhuma za mauaji ya mke wake Mariam Vitaris (19) na mtoto wake wa miaka 2 huku chanzo cha mauaji hayo kikidaiwa ni mgogoro wa kifamilia.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilimu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa mtuhumiwa alitekeleza mauaji hayo usiku wa Agosti 10 mwaka huu ambapo mara baada ya tukio hilo mtuhumiwa alienda kwa kaka yake Salum Said (34) ambaye anaishi katika kijiji hicho kwa lengo la kumuaga kuwa anasafiri na alipomhoji juu ya safari hiyo ndipo alipomueleza kuwa amefanya mauaji hayo nyumbani kwake ndipo kaka yake huyo aliamua kumkamata na kutoa taarifa Polisi.


Wakizungumza kwa masikitiko ndugu wa marehemu ambao ni wakazi wa kata ya Chamwino manispaa ya Morogoro wanaeleza kuwa mtoto wao alifunga ndoa na mume wake ambaye ni mtuhumiwa mwezi wa Julai mwaka huu na kuhamia kijijini huko na kwa kipindi chote hawakuwahi kusikia kama kuna mgogoro unaendelea mpaka kupata taarifa ya mauaji hayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post