JKT YATOA WITO WA VIJANA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA KUJITOLEA MWAKA 2022

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 25,2022 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya vijana watakaojiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea mwaka 2022. Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 25,2022 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya vijana watakaojiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea mwaka 2022.

************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetoa wito kwa vijana wa Tanzania Bara na Visiwani kujiunga na mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa kwa kujitolea kwa mwaka 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 25,2022 Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema utaratibu wa maandalizi ya vijana hao kwaajili ya kujiunga na Jeshi la kujenga Taifa kwa kujitolea unaanza leo hii Agosti 25,2022 na vijana watakaoteuliwa wanatakiwa kuripoti kwenye makambi ya Jeshi la Kujenga Taifa mwezi Septemba 2022.

"JKT linapenda kuwataarifu vijana watakaopata fursa hiyo kuwa halitoi ajira kwa vijana, pia halihusiki kuwatafutia vijana ajira katika Asasi, Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Mashirika mbalimbali ya Serikali na yasiyo ya Kiserikali, bali hutoa mafunzo ambayo yatawasaidia vijana kujiajiri wenyewe mara baada ya kumaliza mkataba wao na Jeshi la Kujenga Taifa". Amesema Brigedia Jenerali Mabena.

Amesema sifa za muombaji anatakiwa awe Raia wa Tanzania, awe na afya njema, akili timamu na asiwe na alama yoyote ya mchoro mwilini (Tattoo), pia mwenye tabia na nidhamu nzuri, hajapatikana na hatia Mahakamani na hajawahi kufungwa.

Kuhusu Elimu , amesema awe na elimu ya darasa la saba umri kuanzia miaka 16 hadi 18, vijana wenye elimu ya kidato cha nne, umri usiwe zaidi ya miaka 20, viajan wenye elimu ya kidato cha sita umri usiwe chini ya miaka 18 na usiwe zaidi ya miaka 22, vijana wenye elimu ya Stashahada umri usuzidi miaka 25, vijana wenye elimu ya Shahada, umri usiwe zaidi ya miaka 26, vijana wenye elimu ya shahada ya Uzamili, umri usiwe zaidi ya miaka 30, vijana wenye elimu ya Shahada ya Uzamivu, umri usizidi miaka 35.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post