POLISI KATAVI WAMKAMATA MWIZI MAARUFU WA PIKIPIKI, ADAKWA NAZO TANO


a
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Ally Hamad Makame akionesha mbele ya wandishi wa Habari pikipiki tano alizokamatwa nazo mtuhumiwa maarufu wa wizi wa pikipiki ambazo alikuwa ameziiba kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi . Picha na Walter Mguluchuma


Na Walter Mguluchuma - Malunde 1 blog

JESHI la Polisi    Mkoa wa Katavi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa maarufu wa wizi wa pikipiki Mkoani Katavi anaefahamika kwa jina la Laurent Lazaro (61) Mkazi wa Kanoge Wilaya ya Mpanda akiwa ameiba pikipiki tano za watu tofauti tofauti.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Ally Hamad Makame amewaambia wandishi wa Habari ofisini kwake mtuhumiwa huyo alikamatwa hapo juzi majira ya saa kumi jioni huko katika Mtaa wa Msufini Kata ya Uwanja wa Ndege Manispaa ya Mpanda.


Kabla ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo jeshi la polisi Mkoa wa Katavi waliandaa msako mkali wa kupambana na uhalifu na waliweza kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na pikipiki ya wizi yenye Namba za usajiri MC 915 CDV aina ya Honlg yenye rangi nyekundu .


Kamanda Ally Makame alisema baada ya mtuhumiwa huyo kukamatwa na kufanyiwa mahojiano ya kina alikiri kuwa aliiba pikipiki nyingine nne kwenye maeneo tofauti tofauti ya Mkoa wa Katavi na aliweza kwenda kuzionyesha pikipiki hiz .


Ambapo katika msako huo walifanikiwa kupata pikipiki hizo nne na kufanya jumla ya pikipiki tano alizokuwa ameiba mtuhumiwa huyo zenye Namba za usajiri MC,445 AAA ina ya SANLG rangi nyekundu , MC 553ADM aina ya SANLG ,MC 468 CUC aina ya SINOREY na MC 802 CQJ aina ya SYNOTEY.

Makame alieleza kuwa huyo alikuwa akiiba kwa kutumia mbinu ya kutembea na funguo bandia ambazo ndizo alikuwa akizitumia kuibia pikipiki zinazokuwa zimepakiwa kwenye maeneo mbalimbali na wamiliki wa pikipiki hizo .


Mtuhumiwa bado anaendelea kuhojiwa ili kuweza kuwapata washiriki wake wanaoshirikiana nae katika kufanya wizi huo wa pikipiki na mara baada ya upelelezi kukamilika mshitakiwa atafikishwa mahakamani akajibu tuhuma zinazomkabili.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post