AKUTWA NA HATIA YA KUMUUA MKE WAKE MIAKA 40 ILIYOPITA
Chris Dowso akiwa na Mkewe Lynette Dowson anayesadikiwa kumuua miaka 40 iliyopita
 **
MWANAUME wa Australia anayefahamika kwa jina la Chris Dawson amepatikana na hatia ya kumuua mkewe miaka 40 iliyopita baada ya podikasti maarufu kuanzisha uchunguzi mpya wa Polisi.Chris Dawson, 74, alituhumiwa kumuua Lynette Dawson mnamo Januari 1982, lakini mwili wake haukupatikana na Dawson ameshikilia kuwa hakuhusika katika kutoweka kwake.


Kesi hiyo ilisikilizwa na umma mnamo mwaka 2018, baada ya kuangaziwa katika The Teacher’s Pet, podikasti ya uhalifu wa kweli, na shinikizo likaongezeka ili uchunguzi ufunguliwe tena.Podikasti hiyo iliweka kisa cha kimazingira kwamba mchezaji huyo wa zamani wa ligi ya raga alimuua mkewe.Siku ya Jumanne, Jaji wa Mahakama Kuu ya New South Wales, Ian Harrison alimpata mwalimu huyo wa zamani wa shule ya upili na hatia ya kumuua mkewe kimakusudi ili kuendeleza uhusiano na kijana aliyekuwa mwanafunzi, ambaye alikuwa amewatunza watoto wake wawili wa kike nyumbani kwake huko Sydney.

Chris Dawson

Mnamo mwaka wa 2018, ripoti za vyombo vya habari, zikinukuu vyanzo vya polisi, zilipendekeza uchunguzi ulifunguliwa tena baada ya utangazaji uliotolewa na podcast, ambayo imepakuliwa mara milioni 30.Hata hivyo, Polisi walisema wakati huo kwamba ilifungua tena uchunguzi baada ya mashahidi wapya kujitokeza.Imeandikwa na Peter Nnally kwa msaada wa mitandao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post