Picha : MAADHIMISHO MIAKA 50 YA WAWATA YAFANYIKA JIMBO KATOLIKI SHINYANGA...KABAKA AONGOZA KUWEKA ALAMA KWA WATAWA


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka, akizungumza kwenye Maadhimisho ya miaka 50 ya Wanawake wa Katoliki Tanzania (WAWATA) Jimbo la Shinyanga.

Picha zote na Marco Maduhu, Amos John na Radio Faraja


Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

WANAWAKE Wakatoliki Tanzania (WAWATA) Jimbo la Shinyanga wameadhimisha miaka 50 ya Chama cha Wananwake Wakatoliki Tanzania WAWATA tangu kuanzishwa kwake mwaka 1972 na kufanya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuweka alama kujenga nyumba ya Watawa.


Maadhimisho hayo yamefanyika leo Agosti 13, 2022 katika Kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akimwakilisha Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson.


Kupitia maadhimisho hayo zaidi ya Shilingi za Kitanzania Milioni 11, zimekusanywa kupitia harambee maalum ya ujenzi wa nyumba ya Watawa wa shirika la kijimbo, la Mtakatifu Bikra Maria Mama mwenye huruma, iliyoendeshwa na Chama cha wanawake Wakatoliki Tanzania WAWATA, Jimbo Katoliki Shinyanga.


Harambee hiyo, imefanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kijimbo ya miaka 50 tangu utume huo wa wanawake uanzishwe hapa nchini.


Akiongoza zoezi la uchangiaji, Mwenyekiti wa umoja wa wanawake (CCM) UWT taifa Mama Gaudensia Kabaka, amesema yeye binafsi anatambua majukumu ya WAWATA katika kanisa na jamii, na amepongeza hatua ya WAWATA jimbo la Shinyanga kukubali kuchukua jukumu la kulilea shirika la Watawa la jimbo.


Mama Kabaka ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwa niaba ya Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson, amewasilisha kiasi cha shilingi Milioni 2 , kilichotolewa na Spika wa Bunge.


“Kwenye Changizo la leo ahadi ni Sh.milioni Tatu na Fedha taslimu ni Sh.milioni 10.5 hivyo endeleeni kufanya machangizo zaidi ili ujenzi wa nyumba ya Watawa ikamilike na kutimiza adhima yenu ya kuweka alama katika maadhimisho haya ya miaka 50 ya WAWATA,”ameongeza.


Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Mhashamu Liberatus Sangu, alitumia nafasi hiyo kumshukuru Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, kupitia mwakilishi wake kukubali kuja kuungana na WAWATA wa jimbo la Shinyanga, katika kusheherekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwa utume wao hapa nchini Tanzania.


Askofu Sangu, amewapongeza WAWATA jimbo la Shinyanga, kwa jinsi wanavyojitoa katika kulitegemeza shirika la Kijimbo la Mtakatifu Bikra Maria Mama mwenye Huruma.


Ameziagiza Parokia zote za jimbo, kuweka utaratibu maalum wa kuendeleza mchakato wa ujenzi wa nyumba hiyo ya Watawa, na kuendelea kuwa na moyo wa kujitegemea na kulitegemeza Kanisa.


Miongoni mwa waliochangia fedha katika harambee hiyo, ni pamoja na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Profesa Siza Donald Tumbo, viongozi mbalimbali wa vyama na serikali pamoja na Waamini.


Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika shughuli mbalimbali Mboneko huku akiwasisitiza wananchi kuhakikisha wanashiriki kwa kikamilifu zoezi la Sensa ya Watu na makazi, linalotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu nchini kote.


Katibu wa Wanawake Katoliki Jimbo la Shinyanga (WAWATA) Beatrice Nangale, amesema umoja huo ulianzishwa mwaka 1972 na leo umetimiza miaka 50, na malengo yake ni kuwaweka wanawake kuwa pamoja na kutimiza utume wao, ikiwamo kuishi kwa Amani, Upendo, kutafuta haki za wanyonge.


Ametaja malengo mengine ni kupinga vitendo vya ukatili, utoaji mimba, uharibifu wa mazingira, pamoja na kupinga mauaji ya vikongwe, na kubainisha kuwa katika ujenzi huo wa nyumba ya Watawa wamepanga kukusanya kiasi cha Sh.milioni 100.


Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo kuu la Arusha Mhashamu Josaphat Lebulu, amesema Wanawake wa Katoliki (WAWATA) kazi yao kubwa ni utume.


Aidha, amewataka kujiamini na kujithamini, kwa kuwa wana mchango mkubwa katika utume wa Kanisa, tangu kuanzishwa kwa chama chao.


Askofu Mkuu Lebulu, ametumia nafasi hiyo kuelezea chimbuko la kuanzishwa kwa utume wa WAWATA miaka 50 iliyopita, na kubanisha kuwa, wamekuwa na mchango mkubwa kupitia karama mbalimbali walizonazo, ikiwemo kuchochea miito ya Upadre na Utawa.


Askofu Mkuu Lebulu, amewataka WAWATA kutambua kuwa, chama hicho siyo chama cha siasa, na badala yake wanapaswa kuzingatia msingi wa kuanzishwa kwake, na kutumia karama walizonazo katika kuujenga ufalme wa Mungu.
Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Arusha Mhashamu Josaphat Lebulu, akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Wanawake wa Katoliki Tanzania (UWAWATA) Jimbo la Shinyanga.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka, akizungumza kwenye Maadhimisho ya miaka 50 ya Wanawake wa Katoliki Tanzania (WAWATA) Jimbo la Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye Maadhimisho ya miaka 50 ya Wanawake wa Katoliki Tanzania (WAWATA) Jimbo la Shinyanga.
Mwenyekiti wa Wanawake wa Katoliki Tanzania Taifa (WAWATA) Evaline Ntenga akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Katibu wa Wanawake Katoliki Jimbo la Shinyanga (WAWATA) Beatrice Nangale, akisoma Risala kwenye maadhimisho hayo.
Mwenyekiti wa (UWT) Tanzania Gaudensia Kabaka, (kulia) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) kwenye maadhimisho hayo. katika Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Ngokolo.
Maadhimisho ya miaka 50 ya (WAWATA) yakiendelea Kanisani.
Maadhimisho ya miaka 50 ya (WAWATA) yakiendelea Kanisani.
Mwenyekiti wa (UWT) Tanzania Gaudensia Kabaka, akishiriki Ibada kwenye Maadhimisho hayo ya miaka 50 ya (WAWATA)
Mwenyekiti wa (UWT) Tanzania Gaudensia Kabaka, awali, akiwa na Askofu wa Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, (kulia) na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, alipowasili kwenye Madhimisho ya miaka 50 ya (WAWATA).
Maadhimisho ya miaka 50 ya (WAWATA) yakiendelea.
Maadhimisho ya miaka 50 ya (WAWATA) yakiendelea.
Maadhimisho ya miaka 50 ya (WAWATA) yakiendelea.
Maadhimisho ya miaka 50 ya (WAWATA) yakiendelea.
Awali wanawake wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwenye Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Ngokolo kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 ya (WAWATA).
Picha zote na Marco Maduhu, Amos John na Radio Faraja blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post