POLISI SHINYANGA WAKAMATA WATU SITA WAKITOROSHA DHAHABU NA MABURUNGUTU MAMILIONI YA FEDHA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha fedha shilingi Milioni 97 (Tsh 97,025,000/= walizokamatwa nazo watu sita wanaotuhumiwa kupatikana wakitorosha madini ya dhahabu yenye uzito wa gramu 930.88 yenye thamani ya shilingi milioni 93 mkoani Shinyanga. Picha na Kadama Malunde


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kukutwa wakitorosha madini ya dhahabu yenye uzito wa gramu 930.88 yenye thamani ya shilingi milioni 93 pamoja na fedha taslimu shilingi Milioni 97.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Alhamisi Agosti 11,2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema tukio hilo limetokea Agosti 10,2022 majira ya tatu usiku katika barabara ya Ilogi kuelekea mkoa jirani wa Geita kata ya Bugarama halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.


“Askari Polisi wakiwa katika doria walilitilia mashaka gari lenye namba za usajili T 913 DRX Toyota Land Cruiser rangi ya njano na kulisimamisha ndani ya gari hilo hilo kulikuwa na watu sita na upekuzi ulipofanyika kwa kushirikiana na Idara zingine za serikali ambapo tulifanikiwa kukuta madini ya dhahabu yenye uzito wa gramu 930.88 yenye thamani ya shilingi 93,000,000/= na pesa taslimu 97,025,000/=”,amesema Kamanda Magomi.


Ameeleza kuwa pia walikuta mzani mmoja wa kielektroniki wa kupimia dhahabu pamoja na mashine moja ya kupima ubora wa dhahabu.


Kamanda Magomi amesema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa watuhumiwa walikuwa wakitorosha madini hayo ya dhahabu kwenda nje ya nchi kwa lengo la kukwepa kodi na tozo za serikali kitendo ambacho ni kosa kisheria.


“Taratibu za kipolisi kama wasimamizi wa sheria zitakapokamilika watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani. Nitoe rai kwa wananchi wanaojihusisha na shughuli za kutafuta kipato kupitia biashara ya madini wafuate sheria zilizopo ili kuinua kipato cha familia na pato la taifa kwa ujumla”,amesema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu watu sita kukamatwa wakitorosha madini ya dhahabu mkoani Shinyanga leo Alhamisi Agosti 11,2022 katika ukumbi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu watu sita kukamatwa wakitorosha madini ya dhahabu mkoani Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha fedha shilingi Milioni 97 (Tsh 97,025,000/= walizokamatwa nazo watu sita wanaotuhumiwa kupatikana wakitorosha madini ya dhahabu yenye uzito wa gramu 930.88 yenye thamani ya shilingi milioni 93 mkoani Shinyanga.
Kushoto ni mashine ya kupima ubora wa dhahabu, mzani wa kielektroniki wa kupimia dhahabu (kushoto) katikati ni madini ya dhahabu yenye uzito wa gramu 930.88 yenye thamani ya shilingi milioni 93 waliyokamatwa nayo watu sita wanaotuhumiwa kutorosha mkoani Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha mashine ya kupima ubora wa dhahabu, mzani wa kielektroniki wa kupimia dhahabu, fedha na madini ya dhahabu yenye uzito wa gramu 930.88 yenye thamani ya shilingi milioni 93 waliyokamatwa nayo watu sita wanaotuhumiwa kutorosha madini mkoani Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi mashine ya kupimia ubora wa madini ya dhahabu waliyokamatwa nayo watu sita wanaotuhumiwa kupatikana wakitorosha madini ya dhahabu yenye uzito wa gramu 930.88 yenye thamani ya shilingi milioni 93 mkoani Shinyanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha mzani wa kielektroniki wa kupimia dhahabu waliokamatwa nao watu sita wanaotuhumiwa kupatikana wakitorosha madini ya dhahabu yenye uzito wa gramu 930.88 yenye thamani ya shilingi milioni 93 mkoani Shinyanga

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

2/Post a Comment/Comments

  1. Pole kwao pia ni ajari kazini kwa watafutaji hao,
    Pia inatakiwa siku nyingine wafuate vigezo tu!

    Walipe tozo za serikali ili kuinua uchumi wa nchi yenye viwanda na uchumi wa kati

    ReplyDelete
  2. Vipi kama walitaka kuuza katika mkoa mwingine??

    ReplyDelete

Post a Comment