HUYU NDIYE ANAYEDAIWA KUWA MREMBO NAMBARI MOJA DUNIANI



Bella Hadid

KULINGANA na ripoti ya hivi majuzi iliyotolewa na “Golden Ratio of Beauty Phi,” Bella Hadid anachukuliwa kuwa mwanamke mrembo zaidi na mwenye sura nzuri, Kila kitu hapa ni kamili, kuanzia kwenye taya, macho ya kuvutia na kuwa na midomo mizuri pamoja na sura inayopendeza.


Mrembo huyo ambaye majina yake kamili ni Isabella Khairiah Hadid, amezaliwa oktoba 9 mwaka 1996 ni mwanamitindo na alishinda tuzo ya mwanamitindo bora mwaka 2016.
Bella Hadid anachukuliwa kuwa mwanamke mzuri zaidi duniani kwa sasa

Bella kitaaluma ni mwanamitindo na anafanya kazi kwenye kampuni zenye chapa kubwa zaidi za mitindo kama vile Tommy Hilfiger, Diane von Furstenberg, na Marc Jacob, Ingawa yeye ni mdogo kuliko dada yake, lakini bado ni mwanamitindo bora, na hisia yake juu ya mitindo ni ya kushangaza.



Katika kipindi cha miaka minnne Hadid amefanikiwa kutokea kwenye majarida ya international Vogue Magazine.

Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post