Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mara Dismas Disusi akizungumza na wanahabari kuhusu tukio hilo
**
Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mara kwa tuhuma za kumuua mwalimu Saidi Hamisi wa Sekondari Masaba iliyopo kijiji cha Nyasirori wilayani Butiama Mkoani Mara na kumjeruhi vibaya Isikaha Hamisi ambae ni mdogo wa marehemu huku wakiwaibia simu za uwakala pamoja na kompyuta.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mara Dismas Disusi amesema tukio hill limetokea usiku wa tarehe 26 mwezi huu ambapo mwalimu huyo alikuwa anatoka katika ofisi yake ya biashara.
Aidha Kaimu Kamanda amesema uchunguzi utakapokamilika watu hao watafikishwa Mahakamani ikiwa ni pamoja na kuwasaka wahalifu wengine ambao wamehusika katika kutenda kosa hilo.