WAZIRI WA MAMBO YA RAIS WA SUDANI KUSINI AWASILI NCHINI

 

Waziri wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia  Prof Adolf Mkenda (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Rais wa Sudani Kusini Dkt Barnaba Marial Benjamin mara alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Waziri wa Mambo ya Rais wa Sudani Kusini Mhe Dkt Barnaba Marial Benjamin.

Na Mathias Canal, KILIMANJARO.

Waziri wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia Prof Adolf Mkenda (Mb)leo tarehe 20 Julai 2022 amempokea Waziri wa Mambo ya Rais wa Sudani Kusini Dkt. Barnaba Marial Benjamin katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Dkt Barnaba amewasili nchini kwa ajili ya kumuwakilisha Rais wa Sudani Kusini Mhe Salva Kiir kwenye Mkutano wa 22 wa Wakuu wa nchi na serikali wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aidha Mkutano huo unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 21-22 Julai 2022 katika ukumbi Ukumbi wa kimataifa wa mikutano-AICC Jijini Arusha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post