WAZIRI MKUU ALITOLEA UFAFANUZI SUALA LA NYONGEZA YA MSHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA

 


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ametoa ufafanuzi juu ya madai ya nyongeza ya mshahara ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wafanyakazi tangu kutoka kwa mshahara wa mwezi Julai.

Pamoja na maelezo mengi kuhusu adhima ya Serikali katika kuboresha maslahi ya wafanyakazi, Waziri Mkuu ameeleza kuwa lengo kubwa la Serikali katika nyongeza ya mshahara imekuwa ni kuwalenga hasa wale wenye kipato cha chini cha mshahara.

“Najua mnajua kwamba tunayo ile Formula inayotumika kwenye upandishaji wa Mishahara, tunaposema tunapandisha mishahara kima cha chini maana yake wanaangaliwa sana wale wafanyakazi wa kipato cha chini, na tukisema kimacha chini kinasaidia sana kupeleka mwelekeo pia hata kwenye sekta binafsi kwamba na huko pia mishahara kima cha chini lazima kianzie hapa.” Amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa ameendelea kwa kusisitiza kuwa ile asilimia iliyotamkwa imewalenga zaidi wale wa kima cha chini, ametoa ufafanuzi kwa kusema kuwa siyo tu kwa wale ambao ndiyo wanaanza kazi lakini hata wale ambao wapo kazini lakini wanapata kima cha chini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments