MAKAMBA AFANYA ZIARA SHINYANGA...AWAHAKIKISHIA WANANCHI HUDUMA YA UMEME HADI VIJIJINIWaziri wa Nishati Januari Makamba (wakwanza kushoto) akiwa ziarani mkoani Shinyanga katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WAZIRI wa Nishati January Makamba amefanya ziara yake ya kikazi mkoani Shinyanga, kwa kuzungumza na viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM), pamoja na kufanya mkutano wa hadhara kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Ngunga wilayani Kishapu, na kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo kwa kupambania maendeleo ya wananchi wake.

Makamba amefanya ziara hiyo ya kikazi leo Julai 19, 2022 akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati pamoja na Wakandarasi kutoka SUMA JKT ambao wanatekeleza mradi wa umeme vijijini (REA).

Akizungumza kwenye ziara yake hiyo amewahakikishia wananchi kuwa Serikali itaendelea kuboresha huduma ya umeme na wananchi wote wataunganishiwa umeme na hadi kufikia 2023 watu wote watakuwa na huduma hiyo.

Amesema Serikali imeendelea kutekeleza miradi ya REA maeneo ya vijijini na umeme utafika maeneo yote kuanzia ngazi ya vitongoji na vijiji kwa sababu umeme ni kichocheo kikubwa cha maendeleo kiuchumi na ndiyo maana Serikali inajitahidi kumaliza changamoto hiyo ya ukosefu ya huduma ya umeme hapa nchini.

Katika hatua nyingine, amempongeza Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo kwa kupambania maendeleo ya wananchi wake na hata kusababisha mradi mkubwa wa umeme wa Jua Megawatts 150 kupelekwa wilayani humo, ambao utaunganishwa pia kwenye Gridi ya Taifa na kumaliza tatizo la umeme.

“Wananchi wa Kishapu mna Mbunge mzuri sana, siyo mpiga kelele Bungeni ni mchapakazi na anapigania maendeleo yenu msije mkamwachia huyu Mbunge yupo kwa ajili yenu, na ndiyo maana hapa Kishapu mmepata mradi mkubwa wa umeme wa Jua nchi nzima,”amesema Makamba.

“Mradi huu utaanza kutekelezwa hivi karibuni na fedha za kulipwa wananchi fidia zimeshapatikana ,na sasa tupo kwenye utaratibu wa kumpata Mkandarasi, na mradi huu wa umeme wa Jua utabadilisha sura ya Kishapu kiuchumi,”ameongeza.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, amesema mradi huo wa umeme wa Jua wanauhitaji sana wilayani humo, ambapo utakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo, pamoja na upatikabaji wa huduma zingine za kijamii kupitia Mfuko wa huduma kwa jamii (CSR) ikiwamo kujengewa Zahanati, Shule na Miradi ya Maji.

Pia ameipongeza Serikali kwa kutekeleza miradi ya umeme wilayani humo, ambapo vijiji 84 vimepata huduma hiyo na kusalia 44 ambavyo navyo vipo kwenye mchakato wa kuunganishiwa umeme.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kupeleka miradi mikubwa ya maendeleo mkoani humo ukiwamo umeme huo wa Jua Megawatts 150.

Aidha, amesema katika Mkoa wa Shinyanga bado kuna tatizo la ukosefu wa huduma ya umeme wa uhakika hasa katika maeneo ya Migodi na viwanda, na kusababisha baadhi ya viwanda kushindwa kufanya kazi na wengine kuzalisha bidhaa kwa zamu sababu umeme haujitoshelezi.

Amesema bado pia kuna tatizo la usambazwaji wa nguzo za umeme ambapo zoezi lake limekuwa la kusuasua, na kuomba huduma hiyo ya umeme iboreshwe haraka ili wananchi wapate huduma ya umeme na wa uhakika na kukuza uchumi wanchi.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Shinyanga Donald Magesa, naye ametoa malalamiko kwa Shirika la umeme Tanzania TANESCO, kuacha tabia ya urasimu hasa kwenye uunganishaji huduma ya umeme kwa wananchi, ambapo wamekuwa wakichukua muda mrefu licha ya kumaliza kulipia gharama zote.

Waziri wa Nishati January Makamba, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ngunga Kata ya Talaga wilayani Kishapu, ambao mradi mkubwa wa umeme wa Jua unatekelezwa katika maeneo yao.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Ngunga Kata Talaga wilayani Kishapu

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungumza na wananchi kwenye mkutano huo.

Diwani wa Kata ya Talaga wilayani Kishapu Richard Dominiko, akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara.

Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa, akizungumza kwenye ziara ya Waziri wa Nishati Januari Makamba.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Nishati January Makamba akiwa ziarani mkoani Shinyanga.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo (kulia) akiteta Jambo na Waziri wa Nishati January Makamba kwenye mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kijiji cha Ngunga wilayani Kishapu.

Wananchi wa Kijiji cha Ngunga wilayani Kishapu wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara wa Waziri wa Nishati Januari Makamba.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.

Wananchi wa Kijiji cha Ngunga wilayani Kishapu wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara wa Waziri wa Nishati Januari Makamba.

Wananchi wa Kijiji cha Ngunga wilayani Kishapu wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara wa Waziri wa Nishati Januari Makamba.

Wananchi wa Kijiji cha Ngunga wilayani Kishapu wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara wa Waziri wa Nishati Januari Makamba.

Awali Waziri wa Nishati Januari Makamba (kulia) akiwa kwenye kikao na viongozi Mbalimbali wa Serikali Mkoani Shinyanga kabla ya kuanza ziara yake, (katikati) ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema na (kushoto) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Waziri wa Nishati January Makamba, (kushoto) akiwa katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Waziri wa Nishati January Makamba, (kushoto) akiwa katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Waziri wa Nishati January Makamba, (kushoto) akiwa katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Waziri wa Nishati January Makamba (katikati) akipiga picha ya Pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema (kulia) na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kushoto)mara baada ya kumaliza ziara yake Mkoani Shinyanga.

Waziri wa Nishati January Makamba (katikati) akipiga picha ya Pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo (kushoto) pamoja na diwani wa Kata ya Talaga wilayani Kishapu Richard Dominiko.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post